Jaji
(R) Mbarouk S. Mbarouk
MAKAMU
MWENYEKITI
TUME
YA TAIFA YA UCHAGUZI
|
Na
Subira Kaswaga (Afisa Habari NEC)
Tume ya Taifa ya Uchaguzi
(NEC) imetangaza tarehe 15, Juni mwaka huu kuwa ni siku ya kufanyika kwa
Uchaguzi Mdogo wa Udiwani katika kata 32 zilizopo katika halmashauri ishirini
(20) za Tanzania Bara.
Akizungumza ofisini kwake
jijini Dar es Salaam Makamu, Mwenyekiti wa NEC Jaji (R) Mbarouk S. Mbarouk
amesema kuwa, Tume imetangaza tarehe ya kufanyika kwa uchaguzi huo baada ya
kupokea taarifa kutoka kwa Waziri mwenye dhamana ya serikali za Mitaa, juu ya
uwepo wazi wa nafasi 31 za Udiwani katika Kata 31 za Tanzania Bara kutokana na
sababu mbalimbali zikiwemo kujiuzulu na vifo.
Aidha, amesema kuwa, Tume
imetangaza kufanyika kwa Uchaguzi Mdogo wa Udiwani katika kata ya Kitangiri
Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela jijini Mwanza sambamba na kata hizo 31, baada
ya Mahakama ya Rufaa kuondoa maombi ya mapitio yaliyowasilishwa katika Mahakama
hiyo, kufuatia kutenguliwa kwa matokeo ya Uchaguzi wa Udiwani katika kata hiyo.
Jaji (R) Mbarouk amesema
kuwa, fomu za uteuzi wa Wagombea zitatolewa kati ya tarehe 27 hadi 31 Mei,
uteuzi wa wagombea utafanyika tarehe 31 Mei, kampeni za uchaguzi zitaanza
tarehe 01 Juni hadi 14 Juni mwaka huu na tarehe 15 Juni, mwaka huu ndiyo
itakuwa siku ya uchaguzi.
Amezitaja
kata zitakazofanya uchaguzi huo kuwa ni Mto
wa Mbu, Mkuyuni na Majengo zilizopo Halmashauri ya Wilaya ya Monduli, Kata za
Ganako, Daa, Mbulumbulu, Oldeani na Kanssay zilizopo katika Halmashauri ya
Wilaya ya Karatu mkoani Arusha. Kata ya Likuyuseka iliyopo Halmashauri ya
Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma.
Kata za Kinyasiti kati
iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa na Kata ya Kikombo iliyopo Halmashauri
ya Manispaa ya Dodoma mkoani Dodoma, Kata ya Itenka iliyopo Halmashauri ya
Wilaya ya Nsimbo mkoani Katavi, Kata za Ipole na Pangale zilizopo Halmashauri
ya Wilaya ya Sikonge na Kata ya Itumba iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Igunga za mkoani Tabora.
Nyingine ni Kata ya Boma
iliyopo Halmashauri ya Mji wa Mafinga mkoani Iringa, Kata za Tandika na Chikongola
zilizopo Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani mkoani Mtwara, Katika Mkoa
wa Dar es Salaam zip Kata za Bonyokwa iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Ilala,
Kata ya Tungi iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni na Kata ya Chang’ombe
iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke.
Pia Kata ya Ruangwa
iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi, Kata za Mkula na Lamadi
zilizopo Halmashauri ya Wilaya ya Busega mkoani Simiyu, Kata za Kibosho
Magharibi na Uru Shimbwe zilizopo Halmashauri ya Wilaya ya Moshi za mkoani
Kilimanjaro, Kata ya Murangi iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Musoma mkoa wa
Mara na Kata ya Siuyu iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi mkoani Singida.
Pamoja na Kata za
Kyaitoke, Mugajale na Ruhunga zilizopo Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba mkoani
Kagera na Kata ya Kitangiri iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela mkoani
Mwanza.
Aidha, Tume ya Taifa ya
Uchaguzi imevikumbusha vyma vya siasa na wadau wote wa uchaguzi kuzingatia
sheria, kanuni, maadili ya Uchaguzi, taratibu, miongozo na maelekezo
yanayotolewa na Tume wakati wote wa kipindi cha Uchaguzi huu mdogo.
MWISHO
Post A Comment: