Na  Heri Shaaban
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amewaomba  Maimamu wa Mkoa wa Dar es Salaam  kuwahimiza Waislam wa mkoa huo kujiandikisha katika daftari la mpiga kura ili waweze kushiriki uchaguzi wa Serikali ya mtaa.
Makonda aliyasema hayo Dar es Salaam leo wakati wa hafla fupi ya ugawaji futari kwa Maimamu ,Watumishi na Makundi maalum.

"Ili tuweze kupambana na mapambano ya rushwa katika Mkoa wangu nawaomba mkajiandikishe ili muweze kuchagua kiongozi bora sio bora kiongozi"alisema.

Makonda alisema viongozi bora wanapatikana kuanzia serikali ya Mtaa  kwani Serikali  bora inanzia serikali ya Mtaa mchague viongozi wasiopenda rushwa.

Alisema hivi karibuni inatarajia kufanyika uchaguzi wa Serikali ya mtaa amewataka waumini wa kiislam kutumia fursa ya kujiandikisha katika daftari mpiga kura.

Alisema mwezi wa Ramadhani ni mwezi muhimu unatukumbusha tuendelee kuishi katika maandiko takatifu  na kujifunza ndani ya mwezi wa Ramadhani.

Aidha alisema katika kipindi cha Ramadhani kuna kuwa na utulivu mkubwa watu wasio waislam pia wanaheshimu.

Pia alitumia nafasi hiyo kuwashukuru Waumini wa Kiislam ni sehemu ya watu walio msaidia katika shughuli mbalimbali.

Aliwataka waumini wa Kiislam kuendelea kuwajenga watoto wao katika misingi ya maadili kwasababu wazazi wengine wanashindwa kuwalea watoto wao katika maadili mema na amewataka Waikristo  kuwaimiza watoto wao kusoma Bibilia.

Kwa upande wake Shekhe wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum alisema kwa niaba ya Shekhe Mkuu wa Tanzania kuwa Sikukuu ya Idd Fitir Kitaifa Mkoa wa Tanga  na Dar es Salaam kimkoa Viwanja vya Mnazi mmoja
Mwisho
Viwanja vya Arnatogolulo
Leo Mei 20/2019
Share To:

Post A Comment: