Mkurugenzi wa Taasisi ya Progress Centre Rose Urio akizungumza kwenye
uzinduzi wa zao la muhogo kitaifa lililofanyika Wilaya ya Kilindi mkoani
Tanga Mei 25, 2019, ambapo mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri wa Kilimo
Omar Mgumba (Picha na Yusuph Mussa).
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shigela akizungumza kwenye uzinduzi wa zao la muhogo kitaifa lililofanyika Wilaya ya Kilindi mkoani Tanga Mei 25, 2019, ambapo mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri wa Kilimo Omar Mgumba (Picha na Yusuph Mussa).
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shigela akizungumza kwenye uzinduzi wa zao la muhogo kitaifa lililofanyika Wilaya ya Kilindi mkoani Tanga Mei 25, 2019, ambapo mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri wa Kilimo Omar Mgumba (Picha na Yusuph Mussa).
Na Yusuph Mussa, Kilindi
TAASISI
ya Progress Centre imewahakikishia wakulima, Serikali na wadau wengine
kuwa zao la muhogo halitakuwa tena kwa ajili ya kujikinga na njaa, bali
kuwa la kiuchumi kwa kuongeza mapato kwa mkulima mmoja mmoja, huku
Serikali ikilitegemea kuongeza pato la Taifa.
Ni
kutokana na zao hilo malighafi yake kutumika kwenye viwanda zaidi ya 60
duniani kwa ajili ya kutengeneza bidhaa mbalimbali. Lakini pia kwa hapa
nchini, baadhi ya viwanda vya bia vimeanza kutumia unga wa muhogo
kutengeneza bia, hivyo ukiacha soko la nje, hata la ndani bado ni kubwa.
Hayo
yalisemwa Mei 25 na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Rose Urio kwenye
uzinduzi wa zao la muhogo kitaifa lililofanyika Wilaya ya Kilindi mkoani
Tanga, ambapo mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri wa Kilimo Omar Mgumba,
huku Wilaya ya Kilindi ikichangia kwa kiasi kikubwa kufanikisha uzinduzi
huo, na tayari ikiwa imewaandaa vilivyo wakulima wake kulima zao la
muhogo.
Urio
ambaye anatumia kauli mbiu ya Cassava For Life (C4L) kuhamasisha zao la
muhogo nchini, alisema mahitaji ya muhogo ni makubwa sokoni, kwani kuna
viwanda tisa vya nguo nchini vinatumia wanga, na nyingi wanaagiza nje
ya nchi. Pia kuna viwanda vya makaratasi zaidi ya vinne nchini
vinavyotumia wanga katika uzalishaji wa karatasi, ambazo tunatumia kila
siku.
"Mgeni
rasmi, kampeni hii inayozinduliwa leo tunategemea italeta matokeo
yafuatayo; mabadiliko ya mtazamo kuhusu muhogo kwamba sio zao la njaa na
umasikini, na ni bidhaa yenye thamani kubwa. Kupunguza umasikini,
kutengeneza ajira, idadi kubwa ya Watanzania kushiriki katika ujenzi wa
Taifa, kuongeza vyanzo vipya vya ulipaji kodi, na kufikia azma ya
Serikali ya Awamu ya Tano ya Tanzania ya Viwanda inayoongozwa na Rais
Dkt. John Magufuli.
"Pia
naomba nieleze kidogo, Cassava Flour (Unga wa Muhogo), viwanda vya bia
vimeanzisha bia itakayotengenezwa na unga wa muhogo. Tuna viwanda tisa
vinavyotumia wanga kwa malighafi, na nyingi inaagizwa kutoka nje. Tuna
viwanda vya makaratasi zaidi ya vinne vinavyotumia wanga katika
uzalishaji wa karatasi tunazotumia kila siku, na mahitaji ya vyakula vya
mifugo ni makubwa sana. Hizo ni baadhi tu ya bidhaa zitokanazo na
mihogo.
Urio
alisema uwepo wa Soko la China ni fursa kubwa. Kampeni itahimiza
uratibu ulio makini ili kuhakikisha wakulima wanafikia soko hili, na
wanunuzi wanapata bidhaa ambayo ni muhogo. Pia watahimiza ufafanuzi wa
mkataba walioingia na China ili wafanyabiashara watakaopenda kwenda huko
wauelewe vema.
Urio
alisema ili kujua na kuona thamani ya jambo hilo, pia watahimiza
matumizi ya kilimo cha mkataba, umuhimu wa kutunza fedha kwa kuweka
akiba, kila mkulima ama kikundi kuwa na kalenda ya kilimo kwa kila
msimu, kujiunga na mifuko ya jamii kama NSSF ili kupata huduma
mbalimbali, umuhimu wa Bima ya Afya, umuhimu wa kuwa na bima ya mazao.
Mgumba
alisema Taasisi ya Progress Centre limefanya jambo zuri kuweza
kuwahamasisha wakulima kuchangamkia zao la muhogo, na wao Serikali
wataweka mazingira mazuri kuona wakulima wanaondolewa mlolongo wa kodi,
ushuru na tozo hasa kwenye pembejeo ili kilimo cha zao hilo kiweze
kuleta tija na waweze kupata faida, kwani ili waweze kupata faida nzuri
kwa zao hilo, wanatakiwa kulima zao hilo kwa kiwango kikubwa.
Awali,
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martin Shigela alisema Serikali imetumia sh.
milioni 200 kwa ajili ya kuwanunulia mbegu za muhogo wakulima, ambapo
kati ya fedha hizo, Shirika la World Vision limetoa sh. milioni 60. Na
katika kuondokana na kilimo cha jembe la mkono, Serikali, kupitia
Shirika la Maendeleo (NDC), wamewakopesha wakulima wa mkoa wa Tanga
matrekta 15, na kati ya hayo, 13 yamekopeshwa wilayani Kilindi.
MWISHO.
Post A Comment: