MBUNGE wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Tanga Ummy Mwalimu ambaye pia ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto akiwa kwenye semina hiyo kulia ni Katibu wa CCM wilaya ya Tanga Salim Kidima akiwa anahesabu fedha zilizotolewa
WANACHAMA wa chama cha Mapinduzi
(CCM) wilaya ya Tanga wametakiwa kujenga mshikamano na umoja miongoni mwao ili
kuweza kuhakikisha wanakiwezesha chama hicho kupata ushindi kwenye uchaguzi wa
Serikali za Mitaa mwaka huu na uchaguzi mkuu mwakani.
Hayo yalisemwa na Katibu
Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi Taifa Humphrey Polepole wakati wa semina ya viongozi wa CCM wa Matawi na Kata
iliyoandaliwa na CCM wilaya ya Tanga kwa kushirikiana Mbunge wa Viti Maalumu
(CCM) Mkoani Tanga Ummy Mwalimu.
Alisema lazima kuwepo mshikamano
ambao utaawasaidia kuweza kuhakikisha wana kuwa wamoja kuelekea kwenye chaguzi
zijazo ili kuhakikisha chama hicho kinaendelea kuwatumikia watanzania kwenye
maeneo mbalimbali hapa nchini.
Aidha pia katika semina hiyo Katibu
huyo alifanya harambee kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya CCM wilaya ya Tanga
ambapo jumla ya shilingi milioni 18 ziliweza kupatikana papo kwa papo huku
Mbunge wa Viti Malumu (CCM) Mkoani Tanga ambaye pia Waziri wa Afya Maendeleo ya
Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akichangia shilingi milioni 5.
Sambamba na uchangiaji huyo lakini
Waziri Ummy alitoa pia bendera za mashina 1000 na sare za chama ili kuimarisha
chama ngazi za chini huku bendera 1000 za mabalozi na tisheti 800 ambazo
watazitumia kwenye shughuli mbalimbali za kichama .
Mwisho.
Post A Comment: