Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Gogo Kata ya Zingiziwa Ramadhani Mapunda akizungumza katika kituo cha Taarifa na Maarifa Sayari wakati wa hafla ya kumpongeza Rais Magufuli na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema kufuatia serikali kutoa mikopo kwa  kikundi cha Sayari Pikipiki tano na Bajaj moja (Kushoto)Diwani wa Viti Maalum manispaa ya Ilala Neema Nyangarilo(Picha na Heri Shaaban)
 Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Gogo Ramadhani Mapunda akimkabidhi pikipiki kituo cha Taarifa na Maarifa Sayari kata ya Zingiziwa mara baada kupokea mikopo ya halmashauri ya Ilala  Kikundi cha Sayari kimefanikiwa kupata pikipiki tano na Bajaj moja  ambapo jana waliandaa hafla ya kumpongeza Rais Magufuli kufanikisha mikopo kwa wajasiriamali waWilaya ya Ilala,(Katikati)Diwani wa Viti  Maalum Manispaa ya Ilala Neema Nyangarilo na Mwenyekiti wa Sayari Nipael Joshua(Picha na Heri shaaban)
 Diwani wa Viti Maalum Manispaa ya Ilala Neema Nyangarilo akikabidhiwa kikapu na Wajasiriamali wa Kituo cha Taarifa na Maarifa Sayari mtaa wa Gogo Kata ya Zingiziwa wilayani Ilala wakati wa Hafla ya kumpongeza Rais John Maguguli kufanikisha kutoa mikopo ya serikali kwa kikundi chao kimefanikiwa kununua pikipiki tano na Bajaj moja (Picha na Heri shaaban)
 Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Ramadhan Mapunda akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo (Picha na Heri Shaaban)
Mwenyekiti wa Kikundi cha Sayari Nipael Joshua akizungumza katika hafla fupi Dar es Salaam leo,ambapo kikundi chao wamefanikiwa kupata fedha za kununua bajaj moja na Pikipiki tano(Picha na Heri Shaaban)
NA HERI SHAABAN
KITUO Cha Taarifa na Maarifa Sayari gruop wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli kwa kuwawezesha , kupata mikopo ya Serikali iliyopitia ngazi ya Halmashauri ya Ilala .

Pongezi hizo za kumpongeza JPM zilitolewa Dar es Salaam leo katika hafla fupi iliyofanyika Kituo cha Taarifa na Maarifa Sayari Kata ya Zingiziwa  Mtaa wa Gogo.

Akitoa salam kwa Rais Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo Ramadhani Mapunda alisema kwa sasa katika Serikali ya awamu ya tano wamepata Rais wa wanyonge kwa kuwawezesha mikopo ya Serikali imewafikia kwa wakati, wananchi wa kipato cha chini waweze kupata fedha za kujishughulisha kibiashara.

"Leo nimealikwa kuwa mgeni rasmi katika taasisi hii ya Sayari wanampongeza Rais Magufuli na Mkuu wa Wilaya ya Ilala , Sophia Mjema  kwa utekekezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi, kuwawezesha wananchi kupata mikopo isiyo na riba ya serikali   ambayo  imetolewa hivi karibuni,  ambapo Sayari wamefanikiwa kupata Pikipiki tano na Bajaj moja"alisema Mapunda.

Mapunda alisema taasisi hiyo ya Sayari inajishughulisha na shughuli mbalimbali,ikiwemo Kilimo cha kisasa  cha (Magolofani)pamoja na kupokea wanawake ambao  wametekelezwa.

Alisema katika Mtaa wa Gogo Kata ya Zingiziwa hicho ndio kikundi kinachojishughulisha kusaidia Jamii kinashirikana na Serikali .

Akielezea changamoto za Mtaa wa Gogo alisema vibanda umiza na majumba ya Danguro ameyatolea taarifa Kata Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Kara inayashughulikia ila mpaka sasa hizo nyumba azijafungwa na taarifa wamepeleka Wilayani.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kituo cha Taarifa na Maarifa Nipael Joshua alishukuru serikali pamoja na viongozi wa Wilaya ya Ilala na Idara ya Maendeleo ya Jamii ya Manispaa  katika mchakato wa kufanikisha kuwapatia fedha zinazopitia ngazi ya halmashauri.

Alisema  kikundi hicho kilianzishwa mwaka 2018 kikiwa na wanachama 19 kwa sasa 76 kinajishughulisha na shughuli mbalimbali zikiwemo za kiuchumi na kijamii.

Nipael alisema Kikundi cha Sayari kinashughulika na kilimo  ,utengenezaji wa Batiki, Sabuni za maji.

Dhumuni la kuanzishwa kwake ni kujikwamua kiuchumi kwa kufanya shughuli mbalimbali za uzalishaji mali na kuacha maisha tegemezi.

Akielezea dhumuni la kituo hicho kuboresha UCHUMI wa afya na kuisaidia watoto walio katika mazingira hatarishi.

Pia kutoa elimu ya Mambo ya jinsia sambamba na kuwahudumia watoto waliokuwa katika mazingira magumu kwa mfano kwa sasa kituo hicho kina kinamuhudumia mwanamke mmoja ambaye alipokelewa akiwa na ujauzito na sasa amejifungua akiwa kituo hicho baada mwanaume kumtelekeza.

"Sisi kama Sayari kituo chetu ni cha kijamii kina shughuli nyingi zikiwemo kupinga rushwa ya ngono na kupinga utekelezaji katika JAMII "alisema Joshua.

Naye Diwani wa Viti Maalum Wanawake Manispaa ya Ilala Neema Nyangarilo aliwataka Wanawake wa Manispaa ya Ilala pia kuunda vikundi vya watu watano watano ambao wanaminiana fedha zipo za Serikali.

Diwani Neema aliwatoa hofu wananchi akiwataka changamkie fursa hiyo ya kusajili vikundi vyao ili waweze kuingia katika mchakato wa kupata mikopo hiyo ambayo inatolewa na Halmashauri ya  ya Ilala kwa Wanawake,Vijana na Watu Wenye Ulemavu ambapo mwezi Mei mwaka huu manispaa inatarajia kutoa mikopo kwa vikundi mbalimbali vilivyotimiza masharti ya uundaji wa Katiba.
 
Mwisho
Kata ya Zingiziwa Mei 19/2019
Share To:

Post A Comment: