Waziri
wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) sambamba na Katibu Mkuu wa Wizara ya
Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe wakiimba wimbo wa mshikamano wakati
akifungua mkutano
wa Baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Kilimo katika ukumbi wa Mikutano
uliopo katika Ofisi za Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) leo
tarehe 24 Mei 2019, wengine pichani ni viongozi wa TUGHE na RAAWU. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akitoa maelezo ya awali wakati akifungua mkutano
wa Baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Kilimo katika ukumbi wa Mikutano
uliopo katika Ofisi za Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) leo
tarehe 24 Mei 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akifungua mkutano
wa Baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Kilimo katika ukumbi wa Mikutano
uliopo katika Ofisi za Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) leo
tarehe 24 Mei 2019, wengine pichani ni viongozi wa TUGHE na RAAWU.
Waziri
wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya
Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe wakiwa katika picha ya pamoja na
wafanyakazi wa wizara ya Kilimo ambao ni wajumbe
wa Baraza la wafanyakazi lililofanyika katika ukumbi wa Mikutano uliopo
katika Ofisi za Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) leo tarehe
24 Mei 2019, wengine pichani ni viongozi wa TUGHE na RAAWU.
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Awamu
ya Tatu ya Mkakati wa Taifa Dhidi ya Rushwa (2017-2022 ina mtizamo mpya
unaolenga kuhakikisha kuwa rushwa inaondolewa nchini kwa kutumia mbinu
mpya na zinazotekelezeka kwa kuweka mkazo katika sekta zenye mazingira
shawishi ya rushwa.
Utekelezaji
wa Mkakati huo unalenga kupunguza na kudhibiti rushwa katika sekta/
maeneo muhimu ya kimkakati ambayo ni pamoja na manunuzi ya umma,
ukusanyaji wa mapato, utoaji wa haki, maliasili na utalii, madini,
nishati, mafuta na gesi, afya, elimu na ardhi.
Rushwa ni adui wa haki, Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) wakati akifungua mkutano
wa Baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Kilimo katika ukumbi wa Mikutano
uliopo katika Ofisi za Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) leo
tarehe 24 Mei 2019 amekemea na kuwataka watumishi kupambana na rushwa
katika sehemu za kazi.
Amewataka
watumishi kuzingatia maadili ya Utumishi wa Umma kwa kutoshiriki katika
kutoa au kupokea rushwa. “Napenda kusisitiza kuwa yeyote
atakayejihusisha na kubainika kupokea au kutoa rushwa hatua stahiki na
kali zitachukuliwa dhidi yake” Alikaririwa Mhe Hasunga
Waziri Hasunga amesema kuwa
bado wizara inakabiliwa na changamoto mbalimbali katika utekelezaji wa
majukumu yake kutoa huduma kwa umma ikiwemo ukosefu wa rasilimali fedha
na rasilimali watu wa kutosha, hali inayosababisha kutofikiwa kwa
malengo. “Niwahakikishie kuwa, Serikali inaendelea kuchukua hatua
mbalimbali za kutatua changamoto hizo. Ni matumaini yangu kuwa, mkiwa
kama Wataalamu mtatumia uwezo wenu katika kuibua mikakati itayosaidia
kuwezesha Kilimo kuwa chenye tija na cha kibiashara” Alisisitiza
Kadhalika, amewataka watumishi wote kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Maadili katika Utumishi wa Umma.
Mhe
Hasunga amesema kuwa serikali haitasita kuchukua hatua kwa Mtumishi
yoyote atakayejihusisha na vitendo vya rushwa pamoja na vitendo
vinavyokiuka maadili ya Utumishi wa Umma.
Serikali
ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais wa Tanzania Dkt John Pombe
Magufuli inayo dhamira ya dhati ya kuondoa uzembe na ubadhirifu miongoni
mwa watumishi wa umma na hivyo mtumishi anaruhusiwa kudai haki zile za
msingi kwa kuzingatia Kanuni, Sheria na Taratibu za Utumishi wa umma wakati wa kutekeleza wajibu wake wa msingi kwa Mwajiri na kwa kutumia lugha ya staha.
Vilevile
serikali inatambua umuhimu wa kuwepo kwa ushirikiano kati ya Mwajiri na
watumishi kwani pasipokuwa na ushirikiano wa pande hizo mbili, ni
vigumu Taasisi kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi. Umuhimu huu wa
mashirikiano, umetiliwa mkazo kupitia Sera, Sheria na Kanuni
zinazosimamia uendeshaji Taasisi za Umma.
Amesema kuwa ili kuweza kutafsiri dhana hiyo,
ni muhimu pia kwa pande zote mbili kutambua haki na wajibu katika
utekelezaji wa majukumu ya kazi, kwani umekuwepo utamaduni wa baadhi ya
watumishi kudai haki bila kutimiza wajibu wao kwa Mwajiri.
MWISHO
Post A Comment: