Makamu
mwenyekiti wa halmashauri hiyo Zakaria Vang’ota akiwa sambamba na kaimu mkurugenzi wa
halmashauri ya Mji wa Mafinga Francis Maghembe waalisema kuwa kupatikana
kwa hati safi katika Halmashauri hiyo kutachochea zaidi kasi ya utendaji kazi
ili kuweza kufikia malengo yaliyokusudiwa
Baadhi ya madiwani na watendaji wa halmasahuri ya Mji wa Mafinga wakifuatilia kwa umakini ripoti ya CAG wakati wa baraza maalum la halmashauri hiyo
NA FREDY MGUNDA,MAFINGA.
HALMASHAURI ya mji wa Mafinga imefanikiwa kupata
hati safi kutokana na utendaji bora,usimamizi wa miradi ukusanyaji
mapato kwenye vyanzo vyake vya ndani katika kipindi cha
mwaka 2018-2019.
Akizungumza kwenye kikao maalumu cha baraza
la madiwani wa halmashauri hiyo kwa lengo la kusoma rasmi taarifa ya CAG kwa
niaba ya mkuu wa mkoa, Kaimu Katibu tawala wa mkoa wa Iringa, Lucas Kambelenje alisema
Halmashauri hiyo imeweza kupata hati safi katika kipindi cha mwaka 2018 -2019
kutokana na watendaji wake wakiwemo madiwani kufanya kazi kwa ushirikiano
katika suala zima la kuhakikisha mapato yanakusanywa kwa kiwango kikubwa
ukilinganisha na kipindi cha nyuma.
‘’Nawapongeza watendaji wa Halmashauri na madiwani kwa kufanya kazi kwa ushirikiano na kufanikiwa kupata hati safi, hivyo nawapongeza muongeze kasi zaidi kiutendaji na kamwe msibweteke,’’alisema
‘’Nawapongeza watendaji wa Halmashauri na madiwani kwa kufanya kazi kwa ushirikiano na kufanikiwa kupata hati safi, hivyo nawapongeza muongeze kasi zaidi kiutendaji na kamwe msibweteke,’’alisema
Aidha aliwataka kufuata misingi imara itayowawezesha kudhibiti mapato na matumizi ya halmashauri kwa kuondoa mapungufu yaliyojitokeza katika kipindi cha nyuma kama kuchelewa kuwasilisha mahesabu kwa mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali(CAG) ,kuchelewa kuwasilisha taarifa za matumizi bila ya kuwa na viambatanishi vya malipo .
‘’Pia epukeni kulipa madeni hewa kwa watumishi ama waliokufa,kuacha kazi ama watumishi watoro sehemu za kazi, kwani kufanya hivyo kutapelekea halmashauri kupata hati chafu.
Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa halmashauri hiyo Zakaria Vang’ota alisema kuwa kupatikana kwa hati safi katika Halmashauri hiyo kutachochea zaidi kasi ya utendaji kazi ili kuweza kufikia malengo yaliyokusudiwa.
‘’Ni dhahiri kila diwani atatekeleza majukumu yake ili kuweza kudhibiti mapato na matumizi ya halmashuari ma kuweza kufanya vizuri zaidi,‘’alisema Vang’ota.
Hata hivyo Vang’ota aliwahimiza madiwani kufanya kazi kwa ushirikiano na kuepuka kufanya kazi kwa mazoea na kuwataka kuwatendea haki wananchi ambao wamewachagua kwa kuhakikisha maendeleo yanawafikia wananchi kwa kuwatataulia kero zinazowakabilia.
Akizungumzia hoja hizo kaimu mkurugenzi wa
halmashauri ya Mji wa Mafinga Francis Maghembe alisema kuwa watahakikisha hoja
zote zinafanyiwa kazi ili kusijitokeze hoja nyingine au kuongezeka kwa madeni
ambayo halmashauri inadaiwa.
Post A Comment: