Naibu
Waziri, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde,
akikambidhi kadi ya CCM aliyekuwa Diwani wa Kata ya Kwembe Manispaa ya
Ubungo, Dweza Horace Kolimba (Chadema) leo jijini Dar es Salaam.
Aliyekuwa
Diwani wa Kata ya Kwembe Manispaa ya Ubuongo, Dweza Horace Kolimba
(Chadema) na aliyekuwa Katibu wa Mbunge wa Kibamba, John Mnyika,
Liberata Samson, wakionyesha kadi zao chama chao kipya cha CCM leo.
Naibu
Waziri, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde,
akizungumza na vijana wa CCM Wilaya ya Ubungo, wakati wa uzinduzi wa
Ubungo ya Kijani Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti
wa UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam, Mussa Kilakala akizingumza katika
mkutano wa Kampeni ya Dar ya Kijani, jijini Dar es Salaam leo
Vijana wa hamasa wa Manispaa ya Ubuongo, wakishangilia jijini Dar es Salaam leo.
………………
Na Ripota Wetu-Michuzi TV
KAMPENI
ya Dar es Salaam ya kijani inayoratibiwa na Umoja wa vijana wa Chama
cha Mapinduzi (UVCCM), imewang’oa Diwani wa Kata ya Kwembe Dweza Horace
Kolimba (Chadema) na Katibu wa Mbunge wa Kibamba John Mnyika, Liberata
Samson kwa kujiunga na CCM.
Akiwapokea
wanachama hao leo jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na
Ajira, ambaye pia ni Mbunge wa Dodoma Mjini, Antony Mavunde, amesema
mwaka 2020 ni lazima majimbo mawili la Ubungo na Kibamba yarudi ndani ya
mikono ya CCM.
Mavunde
amesema kuwa hiyo ni dalili tosha kwamba CCM watachukua majimbo hayo na
ni aibu kuyaacha majimbo hayo mawili yakiwa upinzani.
Amesema
kama makosa yalifanyika hapo awali hategemei tena kurudia tena na
majimbo hayo yakaachwa chini ya John Mnyika (Kibamba ) na Saed Kubenea
(Ubungo), kwa kuwa hakuna wanachokifanya zaidi utekelezaji wa ilani ya
CCM unafanywa na wao.
“Kama
kuna uhitaji wa maji, barabara nzuri vyote vinafanyika sasa kuna haja
gani ya kubakia upande wa pili wa upinzani ni lazima vijana kufanya kazi
kuhakikisha majimbo yanarudi CCM na katika uchaguzi wa serikali za
mitaa kata zote ziwe chini ya chama hicho.
“Jitahidi
hapa viongozi hii ni aibu anzeni na mitaa yote 91 kuhakikisha inarudi
CCM mana hapa nikiangalia hakuna hata pa kupita Mnyika wala Kubenea
watapitia wapi,” amesema Mavunde na kuhoji.
Amesema
jukumu la chama cha siasa ni ushindi na kushika dola na ili ushinde ni
lazima kuishi matatizo ya wanajamii sasa kwa serikali ya sasa
imefanikiwa kwa kiwango kikubwa kutatua changamoto za wananchi wake.
Hata
hivyo amesisitiza kuwa Rais Dk. John Magufuli anakubalika ndani na nje
ya nchi huku akitolea mfano, alipokuwa Afrika Kusini juzi wakati wa
kuapishwa Rais Cyril Ramaphosa, ambapo alishangiliwa na wananchi
wananchi wan chi hiyo.
Katika
hatua nyingine Mavunde amewataka vijana kufanya kazi kwa bidii,
kujiajiri wakati wakisubiri mchakato wa serikali katika kuongeza ajira
kwa vijana hao.
Amewataka
kuhakikisha wanakuwa katika vikundi vya ujasiriamali vya kukopeshana
ili waweze kupata fedha kwani Ubungo ina fedha nyingi ambazo zimetengwa
kwa ajili yao waweze kukopeshwa na kujiendeleza.
Katika
hatua nyingine aliwapongeza Mkoa wa Dar es Salaam kwa kuanzisha kampeni
ya Dar ya Kijani kwa kupandisha bendera ya CCM kila kata.
Kwa
upande wa Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam, Mussa Kilakala,
amesema wanashirikiana vizuri na viongozi wa majimbo ya Ubungo lakini
bado watahakikisha kata zote 14 na majimbo ya Wilaya ya Ubungo zinarejea
CCM kwani ziliazimishwa kwa muda.
“Jimbo
la Ubungo na Kibamba lazima yachukuliwe na CCM mwaka 2020, hakuna
sababu ya kubaki upinzani kwani Rais Magufuli anafanya mambo makubwa
ndani ya CCM na Taifa kwa ujumla.
“Na
hii kampeni ya Dar ya Kijani itaambatana na kazi ya kutundika bendera,
ufunguzi wa matawi kwa kila kata za Mkoa wa Dar es Salaam kuelekea
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa pamoja na Uchaguzi Mkuu mwaka 2020. Hivyo
ni jukumu letu vijana kujipanga na kuhakikisha tunarejeasha heshima ya
chama chetu CCM,” amesema Kilakala.
Post A Comment: