Kaimu Mwenyekiti wa timu ya Lipuli Ayoub Kihwelo akiwa mbele ya waandishi wa habari akielezea lengo la kuitisha harambee ya kuchangia timu hiyo ili kufanikisha kupata fedha za kusaidia kuendesha timu hiyo na kulipa baadhi ya madeni ambayo wa wanadaiwa na wachezaji wa timu hiyo na kuweka mipango kwa ajili ya msimu ujao wa lingu kuu Tanzania bara.
Baadhi ya waandishi wa habari wa mkoani Iringa wakiwasikiliza viongozi wa timu ya Lipuli fc juu ya mipango na mikakati ya Harambee ya kuichangia timu hiyo.

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

UONGOZI wa timu ya mpira wa migu inayoshiliki ligi kuu Tanzania bara Lipuli Fc ya mkoani Iringa umepanga kuitisha harambee ya kuchangia timu hiyo kwa lengo la kuimarisha uchumi kutatua changamoto za mishahara pamoja ada za wachezaji ambazo hadi hii leo bado wanadaiwa na wachezaji wa klabu hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoa Iringa kaimu Mwenyekiti wa timu ya Lipuli Ayoub Kihwelo alisema kuwa lengo la kuitisha harambee hiyo ni kufanikisha kupata fedha za kusaidia kuendesha timu hiyo na kulipa baadhi ya madeni ambayo wa wanadaiwa na wachezaji wa timu hiyo na kuweka mipango kwa ajili ya msimu ujao wa lingu kuu Tanzania bara.

“Ni kweli hatujalipa wachezaji miezi miwili hadi hivi sasa nab ado tunadaiwa pesa za usajili kwa wachezaji wetu hiyo tumeamua kufanya hivyo kwa lengo la kuinusu timu kwa msimu ujao kuondokewa na wachezaji wetu ambao ni wazuri kweli kweli na wanaujua mpira sana” alisema Kihwelo

Kihwelo aliongeza kuwa harambee hiyo itafanyika siku ya jumapili tarehe 7 / 4 / 2019 siku ya jumapili katika ukumbi wa kichangani uliopo manispaa ya Iringa ambapo wanatarajia waziri Mkuu Mstaafu wa awamu ya nne Mizengo  Pinda kuwa mgeni Rasmi

“Siku ya harambee hii tunatarajia waziri Mkuu Mstaafu wa awamu ya nne Mizengo Pinda kuwa mgeni Rasmi akiambatana na wadau mbalimbali akiwepo mkuu wa mkoa wa Iringa pamoja na viongozi mbalimbali wa mkoa huu ambao tunategemea watachangia timu yao ambayo inafanya vizuri katika ligi kuu Tanzania bara” alisema Kihwelo

Kihwelo  alisema wanatarajia kupata zaidi ya shilingi milioni miatatu kwenye Harambee hiyo ambazo zitasaidia kuendesha timu bila kuwa na deni lolote kutoka kwa wachezaji wa timu hiyo na kuweza kupata usajili mpya wa msimu ujao wa ligi kuu Tanzania Bara

“Tunalipa zaidi ya milioni ishirini na nne kila mwezi kwa ajili ya mishahara tu ya wachezaji wa timu na tunagharamia zaidi ya laki tatu kwa siku kwa ajili ya kambi ya timu hivyo utaona kwa namna gani timu inavyogharimu kiasi kikubwa cha fedha na timu hadi hivi sasa haina mdhamini yeyeote yule” alisema Kihwelo

Aliezea kuwa mikakati ya msimu ujao ni kuhakikisha timu inapata mdhamini wa kudumu kwa kuwa timu yetu ya Lipuli imekuwa ikipata matokeo mazuri kila msimu hivyo itatusaidia kupata mdhamini ambaye ataamini kuwa timu hiyo inauwezo wa kuitangazia bidhaa yake.

Kwa upande wake katibu mkuu wa klabu hiyo ya Lipuli Julius Leo ameomba wananchi,wadau wa soka na wapenzi wa klabu ya Lipuli kuichangia timu hiyo kwa kutumia akaunti ya benk ya CRDB  01J2072252000 na kwenye namba ya simu ya MPESA ya timu hiyo ambayo ni 0744 16 24 46 inayojulikana kwa jina la LIPULI FC
Share To:

Post A Comment: