Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akizungumza na Cherie Blair ambaye ni Mke wa Waziri Mkuu wa Zamani wa
Uingereza, Tony Blair walipokutana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Kigali nchini Rwanda April 8, 2019. Majaliwa na Cherie walikuwa wakitoka
kuhudhuria hafla ya kumbukumbu ya miaka 25 ya mauaji ya kimbari nchini humo
iliyofanyika April 7, 2019. Katikati ni Balozi wa Tanzania nchini Rwanda,
Ernest Mangu. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
Waziri
Mkuu akiwa katika picha ya pamoja na Timu ya Serengeti Boys .katika
Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania. Kigali Rwanda April 7/2019
PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU
|
*Asema Watanzania wanamatumaini makubwa kwao, waongeze bidii,
WAZIRI
MKUU, Kassim Majaliwa ametembelea kambi ya timu ya Taifa ya vijana
wenye umri wa chini ya miaka 17 na kuwaeleza kuwa Watanzania
wanamatumaini makubwa dhidi yao, hivyo waongeze bidii.
Alitembelea
kambi hiyo Serengeti Boys iliyoko katika jiji la Kigali nchini Rwanda.
Waziri Mkuu alikwenda Rwanda Aprili 7, 2019 kumuwakilisha Rais Dkt. John
Magufuli kwenye kumbukumbu za miaka 25 ya mauaji ya Kimbari.
Akizungumza
na wachezaji hao jana (Jumapili, Aprili 8, 2019) Waziri Mkuu aliwataka
vijana wanaounda timu hiyo ya Serengeti Boys wahakikishe wanafanya
mazoezi ya kutosha ili waweze kushinda mechi zinazofuata.
“Watanzania
wanamatumaini makubwa dhidi yenu nasi tunazidi kuwaombea kwa Mwenyezi
Mungu muweze kuibuka na ushindi katika michezo yenu iliyobakia
itakayowawezesha kushiriki mashindano ya kombe la dunia.”
Kadhalika,
Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuipongeza timu hiyo ya Serengeti Boys
kwa namna wanavyoitangaza nchi kimataifa kupitia kwenye mashindano
mbalimbali wanayoshiriki na kuibuka na ushindi.
Waziri
Mkuu alisema endapo timu hiyo ya Taifa ya vijana ya Serengeti Boys
itaibuka na ushindi katika michezo yake miwili itakuwa imekata tiketi ya
kushiriki mashindano ya dunia huko nchini Brazil kwa vijana wa umri wa
miaka 17.
Kwa upande wao,
wachezaji na uongozi wa timu ya Serengeti Boys walimkabidhi Waziri Mkuu
kombe walilolipata baada ya kuichapa timu ya Rwanda katika mashindano
maalumu kwa ajili ya kujiandaa na AFCON-U17.
Mashindano
hayo maalumu ya Kimataifa yalishirikisha timu za umri wa chini ya miaka
17 kutoka nchi tatu ambazo ni Tanzania, Cameroon na wenyeji Rwanda,
ambapo Serengeti Boys ilishinda mabao mawili kwa moja dhidi ya Cameroon
na kutoka sare ya mabao matatu kwa matatu na Rwanda.
Pia,
wachezaji hao wamemuahidi Waziri Mkuu kwamba watajitahidi kadiri ya
uwezo wao kuhakikisha wanaibuka na ushidi katika mechi zilizobakia ili
waweze kushiriki kombe la dunia. “Hatutawaangusha Watanzania.”
Awali,
Waziri Mkuu alimshukuru Balozi wa Tanzania nchini Rwanda, Mheshimiwa
Balozi Ernest Mangu pamoja na maofisa wa ubalozi na Watanzania waishio
Rwanda kwa kuendelea kuipa moyo Serengeti Boys.
(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATATU, APRILI 9, 2019.
Post A Comment: