Na Ferdinand Shayo,Kilimanjaro.
Mkuu wa Mkoa
wa Kilimanjaro Dr.Anna Mghwira amewataka Wazalishaji wa mifuko mbadala ambayo
ni rafiki wa mazingira kuchangamkia fursa ya kuzalisha kwa wingi mifuko na kukidhi mahitaji ya mifuko kwani tayari
mkoa huo umepiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki.
Mghira
alisema hayo akitembelea maonyesho ya wiki ya elimu katika uwanja wa Mashujaa
Wilayani Moshi ,amesema kuwa wajasiriamali wanaotumia vifungashio vya mifuko ya
plastiki wanapaswa kujiianda mpaka muda uliopangwa na serikali Mwezi June mwaka
huu waweze kuondokana na matumizi ya plastiki.
“Kwa sasa
mkoa wa Kilimajaro ni marufuku kutumia mifuko ya plastiki tumeanza mapema ili
watu wajiandae ikifika mwezi wa sita mwaka huu watu wawe kwenye mstari na
kuzoea kutumia mifuko mbadala tunashukuru wenzetu wa Harsho Group wameanza
kuzalisha mifuko ya kutosha ” Alisema Dr.Anna
Mratibu wa
Masoko kampuni ya Harsho Group inayozalisha mifuko mbadala,Caroline Satsif alisema kwa mkoa wa Kilimanjaro wamejianda
vyema kuzalisha mifuko ambayo ni rafiki kwa mazingira na kuisambaza kwa bei
nafuu.
Caroline
alisema kuwa wanazalisha mifuko laki 5 kwa siku ambayo inatosheleza mahitaji ya
mkoa wa Kilimanjaro na mikoa jirani pamoja na Tanzania nzima hivyo wamejiandaa
kuzi ba pengo la mifuko ya plastiki.
Anaeleza
kuwa mifuko hiyo inaweza kufuliwa zaidi ya mara tano na iwapo ikitupwa inaweza
kuoza na kuwa mbolea katika ardhi.
Mkazi wa
Manispaa ya Moshi Roman Mnzava alisema kuwa hatua ya Mkoa wa Killimanjaro
kupiga marufuku matumizi ya plastiki utasaidia kuokoa mazingira na hifadhi ya
Mlima Kilimanjaro ambao ni kitovu cha utalii mkoani hapa.
Post A Comment: