Na Humphrey Shao , Globu ya Jamii
Tasisi
ya Utafaiti na sera nchini (REPOA) Itafanya Warsha ya Mwaka kwa
watafiti kote nchini na kutoika mataifa mbalimbali Duniani kwa muda wa
siku mbili kuanzia April 10 Mpaka 11 katika ukumbi wa Ledger Plaza
Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi mtendaji wa
REPOA, Dk. Donald Mmary amesema kuwa katika washa hiyo ambayo itahusisha
mada kuu isemayo 'MAENDELEO YA UCHUMI WA NDANI KATIKA NGAZI YA CHINI'
kama njia kuharakisha mapinduzi ya kimaendeleo nchini Tanzania ambapo
katika mapinduzi hayo watazungumzia mapinduzi ya kilimo na viwanda.
“Nchi
yetu imepiga hatua kubwa kulingana na uchumi kukua lakini bado kuna
maeneo yanayogusa wananchi kuonekana hayajabadilika kwa kasi kwahiyo
wameamua kuliangalia hilo jambo hasa ukuaji wa uchumi katika ngazi ya
chini kuanzia ngazi ya almashauri, vijiji, mitaa na jamii kiujumla”.
Amesema Dk.Mmary.
“Tunatambua
kwamba tunapozungumzia maendeleo ya maendeleo ya ndani kwa ngazi ya
chini tunazungumzia uwezo wa kutambua fursa zilizopo ambazo zinatokana
narasilimali zilizopo hapa nchini”. Amesema Mmary.
amesema
kuwa, ukiachana na suala la kutambua fursa vilevile kunakutafuta mbinu
na mikakati ya kuzigeuza hizo fursa baada ya kuzitambua na kuwa katika
shughuli za kiuchumi.
Pamoja
na hayo kiongozi huyo ameongeza kuwa katika washa hiyo wanaweza
kujifunza kutokana na uzoefu ambao viongozi mbalimbali wamepata ndani ya
nchi kuona changamoto ziko wapi, tunaelekea wapi na tunakosea wapi.
“Tunatambua
kwamba nchi yetu ni kubwa na inavigezo vyote vya saizi na ukubwa wa
idadi ya watu kulingana na nchi nyingine za Afrika”. Mmary ameongeza.Kwa
upande wake mkurugenzi wa tafiti za kimkakati, Jamal Msami amesema kuwa
watakuwa na wawasilishaji wa mada kumi na pia kutakuwa na majukwaa ya
kujadili muunganiko wa uhusiano katika mada na sera za maendeleo ambapo
huko kutakuwa na wataalamu mbalimbali ambao wanaweza wakawa
wajasiliamali, viongozi, wabobezi wa mambo ya taaluma za elimu,
ujasiliamali na masuala ya uwekezaji.
Mkurugenzi
Mtendaji wa REPOA Dkt. Donald Mmary akizungumza na waandishi wa habari
katika ofisi zao zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam
Mwenyekiti
wa Kongamano hilo kutoka REPOA Dkt. Jamal Msami akizungumza na
waandishi wa habari katika ofisi zao zilizopo Mikocheni jijini Dar es
Salaam
Baadhi ya Waandishi wa Habari walioshiriki Mkutano huo wa REPOA wakimsikiliza Dkt. Donald Mmary
Post A Comment: