Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Mamia ya Wanyarandwa
wamekusanyika na kuandamana katika viunga vya jiji la Arusha ikiwa ni ishara ya
kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 25 tangu kutokea kwa mapigano na mauaji ya
Kikabila Nchini na kusababisha mauaji ya maelfu ya Wanyarandwa.
Maadhimisho
hayo yaliyofanyika jijini Arusha yanalenga kuhamasisha umoja na amani miongoni
mwa wanyarandwa kuungana kama taifa bila kujali tofauti za kikabila .
Mwenyekiti
wa Umoja wa Wanyarandwa wanaoishi katika Mataifa mbalimbali duniani Murenzi
Daniel amesema kuwa maadhimisho hayo yanalenga kuwakumbusha kudumisha amani
na umoja kama nguzo muhimu ambayo kwasasa hawako tayari kuipoteza na wanawataka
Wanyarandwa duniani kote kuungana
Tedy
Shungushu ni Mnyarandwa anayeishi jijini Arusha amesema kuwa kumbukumbu hiyo ni
ya muhimu kama taifa kujitafakari na
kuona namna ambavyo wanawakumbuka watu waliowapoteza katika mauaji hayo
na kuwaenzi kila mwaka.
Kwa upande
wao Watanzania walioshiriki katika maadhimisho hayo Maurin Njobi na Omega Urio wamesema kuwa yanawakumbusha kama
Watanzania kudumisha amani na upendo na mshikamano kama taifa ili kuondoa
uwezekano wa matukio kama hayo kutokea nchini
Zaidi ya watu Laki nane wanatajwa
kupoteza maisha kwenye mauaji hayo ya Rwanda nchi ambayo kwa sasa inaongozwa na
Rais wake Paul Kagame.
Post A Comment: