Kamati ya Uchaguzi ya Yanga SC na ile ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) zimefanya mchujo wa awali kwa wagombea katika uchaguzi wa klabu ya Yanga huku Dk Mshindo Msola, Lucas Mashauri na Elias Mwanjala wakipenya kuwania nafasi ya kumrithi Yusuf Manji.

Wagombea waliopitishwa ni Dk Mshindo Msola, Lucas Mashauri na Elias Mwanjala wanaogombea nafasi ya Mwenyekiti.

Wakati Janeth Mbena, katibu mkuu wa zamani wa TFF, Fredrick Mwakalebela, Thobias Lingalangala na Samwel Lukumay wanaogombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti.

Wakati wagombea wa nafasi ya wajumbe ni Ally Sultan, Saad Khimji, Hassan Hussein, Siza Lyimo, Dominick Albinus, Seko Kingo, Hamad Islam, Shafiru Makosa, Injinia Leonard Marango, Cyprian Musiba na Injiani Bahati Mwaseba.

Wengine ni Nassor Matuzya, Abdallah Chikawe, Hussein Nyika, Rodger Gumbo, Said Ntimizi, Palina Conrad, Elius Mkumbo, Suma Mwaitenda, Seif Hassan na Haruna Batenga.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: