Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Joelson Mpina (Mwenye koti
la bluu) akitoa kitambaa kwenye jiwe la msingi kuashiria uzinduzi
wa Kiwanda cha Nyama cha Tan Choice Kibaha mkoani Pwani chenye
uwezo wa kuchinja ng’ombe 100-1500 kwa siku na mbuzi 4000-4500 kwa
siku.
Viongozi wa Tanzania na Misri wakati wa utiaji saini mkataba wa awali
wa ujenzi wa kiwanda cha nyama kwenye ranchi ya Ruvu. Waliokaa kushoto
ni Meneja Mkuu wa Kampuni ya Ranchi za Taifa nchini (NARCO) Profesa,
Philemoni Wambura na kulia ni Mwenyekiti wa Kampuni ya NECAI ya Misri,
Ahmed Hassan Mohamed. Waliosimama mwenye tai nyekundu ni Waziri
wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Joelson Mpina, kushoto kwake ni Balozi wa
Misri nchini Abulwafa, anayefuata ni Meja Jenerali Salah Helmy Abdelmoteleb
na Brigadia Jenerali Mohamed Noureldin. Kulia kwake ni Naibu Waziri
wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega, na Mwenyekiti wa Bodi ya
NARCO Paulo Kimiti.
·
Ni kutokana na mapinduzi makubwa
Wizara ya Mifugo ndani ya mwaka mmoja
Na John Mapepele
Mapinduzi makubwa yanayofanywa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi
katika udhibiti wa magonjwa, bidhaa za mifugo zinazoingia nchini kinyume cha
sheria,uboreshaji wa mbali za mifugo, utoroshaji wa mifugo nje ya nchi, uzalishaji wa mifugo na uzalishaji wa malisho
bora ya mifugo vimeanza kuwavutia wawekezaji wa viwanda vya nyama kuja kuwekeza
na kutoa ajira kwa wanachi na kuchangia kwenye mapato ya Serikali ya awamu ya
tano.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina
kwa nyakati tofauti wakati alipokuwa
akiweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa kiwanda cha nyama cha Tan choice
Tanzania. Kiwanda ambacho ni kikubwa kuliko viwanda vyote Afrika Mashariki na Kati
kinachojengwa Kibaha Pwani na wakati wa utiaji wa saini makubaliano awali baina ya Tanzania na Misri ujenzi wa
miongoni mwa miradi mikubwa barani Afrika wa kiwanda cha uchakataji wa nyama na
utengenezaji wa bidhaa mbalimbali
zitokanazo na Ngozi.
Mpina amesema kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania,
dunia imeshuhudia uanzishwaji wa miradi
mikubwa miwili ya viwanda vya kuchakata
nyama ndani ya wiki moja ambapo kumekuwa na uwekaji wa jiwe la msingi na utiaji
saini wa makubaliano ya ujenzi ambayo itakuwa na manufaa kwa pande zote.
“Ujenzi wa kiwanda cha hiki unapeleka salamu njema kwa nchi
za jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC),SADC,IGAD na mataifa mengine ambayo
inategemea mazao ya mifugo kutoka Tanzania” aliongeza Mpina
Amesema kukamilika kwa viwanda hivyo viwili kutawezasha
kuchinja zaidi ya ng’ombe 3000 mbuzi na
kondoo 10000 kwa siku ambapo pia itatoa ajira za kwa watanzania zaidi ya watu
6000.
“Ilani ya CCM ibala ya 8 (d) na 25(p) inatusisitiza sana sisi
sote tuliopewa dhamana, kuhamasisha sekta binafsi kujenga viwanda vya nyama ili
kuongeza thamani na kukuza uchumi wa nchi na wadau katika mnyororo mzima wa
thamani” alisisitiza Mpina kwenye hotuba yake ya uwekaji wa jiwe la msingi
kwenye kiwanda cha Tan Choice
Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha nyama cha Tan choice
Tanzania Rashid Abdilah ameishukuru Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kutoa
miongozo na ushirikiano wa karibu ambao umewawezesha
kujenga kiwanda na kufikia asilimia 85 ndani ya miezi sita na kuahidi kukamilisha
kiwanda hicho na kuanza uzalishaji ifikapo agosti 2020.
Akizungumza mara baada
ya kushuhudia utiaji wa saini
makubaliano ya awali ya kiwanda cha “Ruvu Intergrated Industry” Waziri Mpina
amesema kiwanda hicho ni cha aina yake, ambapo ngombe wazima
wataletwa na kupumzishwa katika eneo maalum kabla ya kuchinjwa(holding ground) hatimaye
watachinjwa na mwisho kupata nyama yenye kiwango cha kimataifa(ISO) na
hadhi ya kuwa na ithibati ya “halal”.
Aidha amesema kiwanda hicho kikianza kufanya kazi kitafanya
kazi ya kutengeneza bidhaa nyingine za
mifugo kama mikanda mikoba na viatu na chakula cha mifugo.
Amesema asilimia 1.4 ya mifugo yote duniani inapatikana
Tanzania na asilimia 11 ya mifugo yote
Afrika ipo Tanzania hivyo kuna uhakika wa malighafi ya kutosha kwa ajili ya viwanda vinavyoanzishwa ambapo
alitoa muda usiozidi miezi mitatu
kwa timu ya wataalam wa Tanzania na Misri
kukamilisha mara moja na upembuzi
yakinifu ili mkataba rasmi wa ubia (Joint Venture Agreement) na uendeshaji wa kiwanda
uwe umesainiwa.
Aidha, Mpina aliiomba Serikali ya Misri kuendelea kuwekeza
katika maeneo mengine ya mifugo na uvuvi
hususan katika uendeshaji wa
shirika la Uvuvi Tanzania(TAFICO) ambalo
Serikali tayari imeshalifufua, Hiifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu, viwanda
vya kuchakata samaki, ufugaji wa samaki baharini na maji baridi.
Amesema fursa za uvuvi
wa ukanda wa uchumi wa Bahari Kuu(EEZ)
ni kubwa kwa Tanzania kuwa eneo la kilomita 223,000 unafaa kwa ajili ya uvuvi
wa samaki aina ya Jodari na utalii wa majini unaojali mazingira.
Kwa upande wake Balozi wa Misri Abulwafa amesema hatua ya
uwekaji wa saini hati ya makubaliano hayo ni kielelezo cha ushirikiano
uliodumu kwa zaidi ya miaka 50 baina ya
nchi zote mbili.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Kilimo, Mifugo na
Maji Mahmoud Mgimwa na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Pwani Ramadhani Maneno
walipongeza hatua ya Wizara ambapo walisema kuwa wizara inatekeleza
Chimbuko la mradi ujenzi wa kiwanda cha Ruvu ni kutokana na
mashirikiano mazuri na majadiliano baina ya Rais Dk.John Pombe Joseph Magufuli
na Rais wa Misri Abdel Fattah El
Sis yaliyofanyika Agosti 2017 na pia kufuatia
kikao cha ujumbe wa Waziri wa Mifugo wa Misri Desemba 2018 na Waziri
Mpina ofisini kwake jijini Dodoma.
Utiaji wa saini kwa mradi huo umefanywa na Meneja Mkuu wa
Kampuni ya Ranchi za Taifa(NARCO) Profesa Philemoni Wambura na Mwenyekiti wa
Kampuni ya NECAI ya Misri, Ahmed Hassan Mohamed katika hafla iliyofanyika
kwenye Ofisi ndogo za Wizara ya Mifugo
jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Mwanzoni mwa wiki hii, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania,Mheshimiwa John Pombe Joseph Magufuli amewaagiza viongozi wote nchini
kuhakikisha wanaondoa vikwazo vyote dhidi ya wawekezaji ambao
wanadhamira ya dhati ya kuwekeza katika maeneo mbalimbali ya kuimarisha uchumi, kuzalisha ajira,
kuongeza mapato ya Serikali na kustawisha
maisha ya wananchi wakati akifunguakiwanda cha kubangua Korosho chaYalin
Cashenut Company Ltd kilichopo eneo la
Msijute Mtwara vijijini.
Post A Comment: