,
Muonekano
nyanya katika moja ya vitalu nyumba vilivyotembelewa na Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria katika Wilaya ya Dodoma mjini.
Mkurugenzi
wa Ajira kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu
Bw. Ally Msaki akiwa kwenye moja ya kitalu nyumba wakati wa ziara ya
Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria katika Wilaya ya Dodoma mjini na
Chamwino.(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU & MAELEZO)]
Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Antony Mavunde
akisisitiza jambo wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba
na Sheria wakati wa ziara ya kamati hiyo kutembelea mradi wa ujenzi wa
vitalu nyumba katika Wilaya ya Chamwino Jijini Dodoma Aprili 06, 2019.
Moja
ya Kitalu Nyumba cha mafano katika Wilaya ya Chamwino kama
Kinavyoonekana ikiwa ni moja ya mikakati ya kuwainua vijana kupitia
programu ya uwezeshaji inayotekelezwa na Ofisi ya Waziri Mkuu.
Sehemu
ya Vijana zaidi ya 100 wa Wilaya ya Chamwino walionufaika na Programu
ya ujenzi wa vitalu nyumba katika kila halmashauri hapa nchini wakiwa
katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa Kamati hiyo.
Makamu
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Mhe. Nagma
Giga akizungumza wakati wa ziara ya wabunge wa kamati hiyo Wilayani
Chamwino Jijini Dodoma, kujionea utekelezaji wa Programu ya ujenzi wa
vitalu nyumba katika kila halmashauri hapa nchini.
Mtendaji
Mkuu wa Kampuni ya Holly Green Agric Mhandisi Octavian Lasway akitoa
maelezo kwa wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria
kuhusu namna walivyoweza kutekeleza Programu ya ujenzi wa vitalu nyumba
katika halmashauri ya Wilaya ya Chamwino pamoja na kuwajengea uwezo
vijana ili kufanya mpango huo unaotekelezwa na Ofisi ya Waziri mkuu.
Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Antony Mavunde
akiwa pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba
na Sheria Mhe. Nagma Giga wakiwa ndani ya moja ya vitalu nyumba hivyo.
Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi (Wenye Ulemavu) Mhe. Stella IKupa
akifurahia jambo na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Katiba na Sheria Mhe. Nagma Giga akizungumza wakati wa ziara ya wabunge
wa kamati hiyo Wilayani Chamwino Dodoma kujionea utekelezaji wa Programu
ya ujenzi wa vitalu nyumba.
Mmoja
wa wanufaika wa programu ya ujenzi wa vitalu nyumba na mafunzo ya
kuwawezesha vijana kutumia ujuzi huo kujikwamua kiuchumi akipongeza
juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano kuiwawezesha vijana.
Sehemu ya miche ya nyanya katika kitalu nyumba kama inavyoonekana katika picha ikiwa tayari kumika katika kitalu nyumba.
Wanufaika
wa programu ya kukuza ujuzi eneo la kilimo cha kisasa kupitia
teknolojia ya kitalu nyumba “green house” wameipongeza Serikali kwa
kuendelea kuwawezesha katika masuala ya kilimo hicho na kujikwamua
kiuchumi.
Pongezi
hizo wamezitoa hii leo Aprili 06, 2019 wakati wa ziara ya Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria ilipotembelea kukagua utekelezaji wa
Programu ya ukuzaji ujuzi kwa vijana katika Wilaya ya Chamwino Jijini
Dodoma.
Katika
kupongeza jitihada hizo wanufaika wa programu ya kilimo hicho
walibainisha mafanikio ikiwemo, kupata ujuzi wa kilimo cha mazao
mbalimbali, kujikwamua kiuchumi ikiwa ni sehemu ya kujipatia vipato
halali pamoja na kusaidia upatikanaji wa ajira kwa vijana wanaowezeshwa
elimu hiyo.
Mtaalam
kutoka kampuni ya Holly green Bw. Octovian Lasway alieleza kuwa, zaidi
ya vijana 100 wamenufaika na elimu ya kilimo cha kitalu nyumba katika
Wilaya hiyo na kusaidia kuondokana na changamoto za ukosefu wa ajira
nchini.
“Programu
hii imekuja wakati sahihi na imesaidia kundi kubwa la vijana kwa
kuzingatia mafanikio yatokanayo na kilimo hiki cha kisasa kinacholeta
tija kwa kuwa na mazao bora na kuongeza kipato kwa wananchi,”alisisitiza
Octovian.
Akitoa
maelezo kwa wanufaika hao, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu
anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe.Anthony Mavunde alieleza
jitihada za Serikali katika kufikia kundi kubwa la vijana katika
kuwawezesha na kuwajengea uwezo wa masuala ya ukuzaji ujuzi ili
kuendelea kuongeza tija na kujikwamua kiuchumi kwa kuzingatia falsafa ya
uchumi wa viwanda.
“Mradi
umekusudiwa kutekelezwa kwenye Halmashauri zote 185 Tanzania Bara
ambapo awamu ya kwanza itafikiwa mikoa 12 na Halmashauri 83 kwa lengo la
kuwezesha vijana kuwa na ujuzi pamoja na stadi za maisha ili kufikia
malengo tuliyojiwekea kama Serikali,”alieleza Mavunde
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Ajira wa ofisi hiyo Bw.Ally Msaki alieleza
kuwa, mradi huo ni sehemu ya utekelezaji wa mkakati ya Serikali katika
kutatua changamoto ya ajira kwa vijana na kuboresha kipato kwa
watanzania.
“Mpango
huu unalenga kufikia vijana 18800 nchi nzima ambapo kila Halmashauri
itafikia vijana 100 na hadi sasa tumefikia halmashauri za mkoa 10,
ikiwemo;Dodoma, Iringa, Mbeya, Ruvuma, Lindi, Mwanza, Simiyu, Geita,
Shinyanga na Kagera,”alieleza Msaki
Naye
Makamu mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Nagma Giga alifurahishwa na
utendaji na bidii ya vijana hao na kuwaasa kuendelea kutumia ujuzi huo
kwa vijana wengine nchini.
Naye
Naibu Waziri wa Ofisi hiyo anayeshughulikia Watu Wenye Ulemavu
Mhe.Stella Ikupa aliwataka vijana kutodharau kilimo kwa kuzingatia
mchango wake katika kujikwamua kimaisha.
“Maisha
hayapo kwenye karamu peke yake bali jembe linauwezo wa kuwatoa na
kuwakwamua kiuchumi endapo kutakuwa na umakini na kujitoa kwa
bidii,”alisisitiza Ikupa.
Kwa
upande wake mwanagenzi Bw.Festo Ezikiel aliendelea kuipongeza serikali
kuendelea kuwaamii na kuwajengea uwezo wa kilio cha kisasa cha kutumia
kitalu nyumba.
“Tunaipongeza
Serikali kutuamii na kutupa ujuzi kuhusu kilimo hiki nasi tunaahidi
kushirikisha vijana wengine waliopo katika maeneo yetu ili kujikwamua
kiuchumi,”alisema Ezekiel
=MWISHO=
Post A Comment: