Aliekuwa Mwenyekiti wa kijiji cha Ngyani kata ya Nkwaranga Ndugu Elishilia mathayo Ngyeve wa chama cha demokrasia na Manendeleo CHADEMA amejiuzulu nafasi yake ya uenyekiti na kujiunga na chama cha mapinduzi CCM katika mkutano wa hadhara wa mkuu wa wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Muro katika kata ya Nkwaranga.
Ndugu Ngyeve amepokelea na mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Meru Comrade Laizer ambae amesema ujio wa wenyeviti wengi wa Chadema kuja ccm ni dalili tosha ya chama cha mapinduzi kukubalika katika Wilaya ya Arumeru ambapo amesema endapo kasi hiyo itaendelea ni dhahiri kuwa chama cha mapinduzi ccm kitakwenda kushinda kwa kishindo viti vyote vya uenyekiti wa vijiji na vitongoji unataorajiwa kufanyika mapema mwaka huu.
Post A Comment: