Hayo yalisemwa leo na Meneja wa Tanesco mkoani Tanga Mhandisi Julius Sabu alisema wizi huo wa waya za shaba umekuwa ukifanyika kwa kukatwa waya hizo zinazotoka kwenye transfoma kwenda ardhini ambazo zinawekwa maalumu kwa ajili ya kuizuia isiungue.
Alisema kibaya zaidi ni watu wamekuwa wakiiba waya kwenye juu righting arrest na kusababiusha transfoma ziiungue huku akieleza mwishoni mwa waka jana kuna mvua ziliambatana na radi na upepo mkali ambapo walipoteza transfoma nane ambazo zilipelekea wao kuingia hasara ya milioni 120 kwa ajili ya kubadilisha transfoma hizo.
Meneja huyo alisema kati hasara ya zaidi ya milioni 100 unatokana na uharibifu wa miundombinu ya nguzo kwa kuchomwa moto na wananchi kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo Muheza, Korogwe, huku Shirika hilo likilazimika kupeleka wataalamu wake kwa ajili ya kurejesha miundombinu hiyo.
“Ukiangalia kati ya nguzo hizo 100 kwa wilaya ya Muheza ni nguzo 28 zimechomwa moto, Korogwe 21 na Handeni 9 na kilindi zaidi ya nguzo 50 kudondoka kwa kuchomwa moto na watu wasiojulikana na hivyo kusababisha tatizo la umeme kwenye “Alisema Meneja huyo.
“Licha hya hasara hizo lakini pia tulipoteza fedha tulizopaswa kukusanya pia usumbufu ulitokea kwa wateja kukaa giza niwaombe raia wema wateja na wananchi watusaidia kuwafichua watu wanaoiba vifaa hivyo”Alisema Meneja huyo
“Ukiangalia waya za kopa ni ndogo ambazo hazifiki hata milioni moja lakini watu hao wanapoziiba wanasababisha kupoteza transfoma ya zaidi ya milioni 10 wananchi watusaidia kutoa taarifa Polisi au tanesco wakibaini watu wanauza waya hizo kwenye maeneo yao”Alisema
Aidha alisema kwa wilaya ya Muheza walifanikiwa kukamata baadhi ya watu ambao walifikishwa mahakamani mmoja alihukumiwa miaka mitatu, mmoja miaka mmoja na mwengine bado kesi inaendelea, wizi wa mafuta ya transfoma wananchi muheza walifanikiwa kumkamata mwiizi
Mwisho.
Post A Comment: