Spika wa Bunge, Job Ndugai amemtahadharisha Mbunge wa Arusha mjini Godbles Lema kuwa pamoja na adhabu aliyopewa na Bunge, akiendelea kulidhalilisha Bunge ataitwa tena kwenye Kamati ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge na kuhojiwa.
Mapema leo Kamati ya Bunge ya Kinga, Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge imemtia hatiani Mbunge huyo kwa kudharau Bunge kwa kuita Bunge ni dhaifu na hivyo kamati imeazimia Lema kutohudhuria mikutano mitatu ya Bunge.
Wakati huo huo, Spika Ndugai amewaagiza maaskari wa Bunge kuhakikisha wabunge wote waliosusia kikao cha Bunge na kutoka nje hawarudi Bungeni tena kwa siku ya leo.
Post A Comment: