Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea taarifa ya utendaji ya Chama cha
Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kimataifa (CPA - INERNTIONAL) ya mwaka
2018 kutoka kwa Naibu Spika wa Bunge la Cameroon na Mwenyekiti wa
Kamati ya Utendaji ya CPA, Mhe. Emilia Monjowa Lifaka, baada ya
mazungumzo yao, ofisini kwa Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma Aprili 4,
2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Naibu Spika wa Bunge la Cameroon na Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kimatifa (CPA-INTERNATIONAL), Mhe. Emilia Monjowa Lifaka, ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dodoma, Aprili 4, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Naibu Spika wa Bunge la Cameroon na Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kimatifa (CPA-INTERNATIONAL), Mhe. Emilia Monjowa Lifaka, ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dodoma, Aprili 4, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Naibu Spika wa Bunge
la Cameroon na Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya Chama cha Mabunge ya
Jumuiya ya Madola Kimatifa (CPA-INTERNATIONAL), Mhe. Emilia Monjowa
Lifaka, ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dodoma, Aprili 4, 2019. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Naibu
Spika wa Bunge la Cameroon na Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya Chama cha
Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kimatifa (CPA-INTERNATIONAL), Mhe. Emilia
Monjowa Lifaka (wa pili kushoto) baada ya mazungumzo yao, ofisini kwa
Waziri Mkuu jijini Dodoma, Aprili 4, 2019. Wa tatu kulia ni Mbunge wa
Babati Vijijni, Mhe. Vrajilal Jitu Son na wa pili kushoto ni Mbunge wa
Viti Maalum na Mwakilishi wa CPA tawi la Tanzania, Mhe. Maria Kangoye.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema Serikali itatoa ushirikiano kwa Maspika wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika (CPA – Africa)
wanaotarajia kufanya mkutano wao Novemba 2019, nchini Tanzania.
Ametoa
kauli hiyo jana (Alhamisi, Aprili 4, 2019) alipokutana na kufanya
mazungumzo na Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya Chama cha Mabunge ya Madola Kanda ya Afrika, Mheshimiwa Emilia Monjolwa Lifaka.
Waziri
Mkuu alisema Bunge na Serikali nchini wanafanya kazi kwa kushirikiana,
hivyo amemuhakikishia Mhe. Emilia ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge la
Cameroon kuwa Serikali itatoa ushirikiano unaohitajika kwa CPA ili
kufanikisha malengo tarajiwa
Pia,
Waziri Mkuu alisema Serikali inaushukuru uongozi wa CPA kwa kutoa
ushirikiano stahiki kwa wabunge wa Bunge la Tanzania ambao ni wanachama
wa CPA
Kwa upande wake,
Mhe. Emilia aliipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuzingatia usawa wa
kijinsia na kutoa fursa kwa wanawake katika nafasi za uongozi ikiwa ni
pamoja na idadi kubwa ya wabunge wanawake kufikia asilimia zaidi ya 30
ya wabunge wote.
Kadhalika, Mwenyekiti huyo alisema Maspika wa CPA – Afrikawanaotarajia
kufanya mkutano Novemba 2019, katika jiji la Arusha nchini Tanzania
wameridhika sana kwa ahadi ya Serikali ya Tanzania kuhusu ushirikiano na
maandalizi mazuri.
Mkutano huo wa Maspika wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika utajadili ajenda mbalimbali pamoja na kuimarisha ushirikiano uliopo kati ya nchi hizo kwa maslahi ya vizazi vya sasa na vijavyo.
(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
41193 – Dodoma,
IJUMAA, APRILI 5, 2019.
Post A Comment: