Na. Amiri kilagalila, Njombe

Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt.John pombe Magufuli,anatarajia kufanya ziara ya siku mbili mkoani Njombe baada ya kutokea mkoani Ruvuma na kukagua baadhi ya miradi mikubwa ikiwemo ya barabara na hospital.

Akizungumza na vyombo vya habari ofini kwake, Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Olesendeka amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Dkt.John Pombe Magufuli atafanya ziara ya siku mbili kuanzia tarehe 09-10/04/2019.

Olesendeka amesema kuwa katika Ziara hiyo atatembelea na kuzindua miradi mbali mbali ya maendeleo na kuongea na wananchi.

“Mheshimiwa Rais siku ya kwanza atapokelewa na viongozi wa serikali, chama pamoja na wananchi katika mpaka wa mkoa wa Njombe na mkoa wa Ruvuma na baada ya hapo atakwenda kuweka mawe ya msingi katika miradi mikubwa miwili,mradi wa kwanza itakuwa ni kuweka jiwe la msingi kwenye hospital ya Rufaa ya mkoa,awamu ya kwanza imekamilika kwa upande wa huduma za wagonjwa wa Nje (OPD) na imegharimu kiasi cha Tshs.Bilioni 3.6”alisema Olesendeka.

Aidha ataweka jiwe la Msingi katika barabara ya Njombe-Moronga-Makete  inayojengwa kwa kiwango cha lami kwa gharama ya takribani Tshs.Bilioni 217 ikiwa ni moja kati ya miradi ya barabara za lami na zege zinazojengwa mkoani Njombe yenye thamani ya zaidi ya Tshs.Bilioni 480 pamoja na kufanya mazungumzo na wananchi katika viwanja vya shule ya msingi Ramadhani.

Katika hatua nyingine Olesendeka amesema kuwa  siku ya pili ya ziara ya Rais Magufuli atafungua kiwanda cha chai cha UNILIVER (kabambe factory)

“Siku inayofuata tarehe 10 ya mwezi wa 4 mheshimiwa Rais atafanya kazi ya kukaguwa miradi mikubwa miwili,mradi wa kwanza utakuwa ni wa kiwanda cha kabambe Tea factory inayomilikiwa na kampuni ya Uniliver  Plc ya London nchini Uingereza  kwa pamoja na kampuni ya Uniliver  nv ya Roturdam nchini Netheland, mchana atapata fursa ya kufungua mradi wa ujenzi wa barabara ya Mafinga-Makambako-Igawa eneo la mpaka wa Makambako na wilaya ya Wanging’ombe ambao ni kilometa 64.6 uliojengwa kwa kiwango cha lami ya kisasa na kugharimu Tshs.Bilioni 103,432,947,407.64 na baadaye katika viwanja vya makambako  atapata fursa ya kuzungumza na wananchi wa Makambako na Njombe kwa ujumla”alisema Olesendeka

Kutokana na umuhimu wa ziara hiyo Olesendeka ametoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Njombe na mikoa jirani ya Mbeya na Iringa kujitokeza kwa wingi katika maeneo ambayo miradi itazinduliwa pamoja na mikutano ya hadhara ili kumlaki na kumsikiliza Rais na kiongozi huyo wa kitaifa.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: