Kamishna Mkuu wa kudhibiti fedha haramu hapa nchini Onesmo Makombe akizungumza na waandishi wa habari
Na Woinde Shizza, Globu ya jamii
NCHI
za kusini na mashariki mwa Afrika zimetakiwa kuhakikisha kuwa zinabuni
mbinu mbadala kuhakikisha kuwa zinakabiliana na tatizo la fedha haramu
ambalo limekuwa likizidi kushika kasi katika nchi hizo.
Kamishna
Mkuu wa kudhibiti fedha haramu hapa nchini Onesmo Makombe ameyasema
hayo jijini Arusha jana alipokuwa akifungua mkutano wa maofisa wa
kupambana na fedha haramu kutoka nchi za kusini na mashariki mwa Afrika.
Amesema
kuwa suala la fedha haramu limekuwa ni changamoto kubwa katika nchi
hizo na kueleza kuwa endapo juhudi makini hazitachukuliwa kukabiliana
na tatizo hilo,itasababisha uchumi wan chi hizo kuzidi kushuka.
‘’Serikali
za nchi wanachama zitatakiwa kukabiliana na biashara haramu za
binadamu,madawa ya kulevya,rushwa na mengineyo yanayofanana nahayo kwani
mambo hayo ndiyo yamekuwa yakichangia kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa
fedha haramu”alisema Makombe.
Ameshauri
kila nchi mwanachama wa umoja wa kupambana na fedha haramu kwa nchi za
kusini na mashariki mwa Afrika kuhakikisha kuwa itatunga sheria kali za
kuhakikisha kuwa zinawabana wale wote wanaojihusisha na fedha haramu.
Awali,Mtendaji
Mkuu wa kitengo cha kudhibiti fedha haramu hapa nchini,Eliamani Kisanga
alisema kuwa lengo la mkutano huo ni kutengeneza sera na sheria za
zitakazojikita zaidi kuhakikisha kuwa
nchi hizo zinakabiliana kikamilifu na tatizo hilo.
Amesema
kuwa pia katika mkutano huo watajadili kwa kina ili kuhakikisha kuwa
sheria zinazotumika kukabiliana na fedha haramu katika nchi wanachama
zinafanana ikiwa ni pamoja na wahusika wanaopatika na makosa hayo kupewa
adhabu zinazolingana katika nchi hizo.
Amesema
kuwa mkutano huo utakaofanyika kwa juma moja unashirikisha nchi
wanachama kumi na nane ambao unahudhuriwa na wajumbe zaidi ya mia mbili
kutoka katika nchi hizo na kwamba mada mbalimbali zitawasilishwa na
wajumbe watapata fursa ya kubadilishana uzoefu.
Alizitaja
baadhi ya taasisi zinazoshiriki katika mkutano huo kuwa ni maofisa wa
taasisi za kupambana na fedha haramu kutoka nchi wanachama,idara za
mahakama,polisi,waendesha mashitaka,mamlaka za usimamizi wa bima,mabenki
na malaka za kupambana na rushwa kutoka nchi
husika.
Post A Comment: