Na Heri Shaaban
 NAIBU Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto amesema  maendeleo ya nchi yeyote yanaitaji Taifa liwe na elimu bora na kukuza uchumi imara.

 Kumbilamoto  ambaye kwa sasa ndio Kaimu MEYA manispaa ya Ilala alisema hayo, wakati alipokuwa akikabidhi mashine photopy kwa shule ya msingi Kombo Vingunguti Wilayani Ilala.

"Taifa lolote ili liweze kuwa na Maendeleo lazima wananchi wake waweze kupatiwa elimu bora itakayo wawezesha kukuza uchumi wa viwanda  "alisema Kumbilamboto..

Kumbilamoto alisema   katika juhudi za kumsaidia Rais  wa awamu ya tano katika upande wa sekta ya elimu  amekabidhi mashine ya Photokopy ili iwawezeshe kudurufu mitihani ya shule zilizopo kata ya Vingunguti msaada uliotolewa na wadau wa sekta ya elimu Kampuni ya MMP.

Alisema katika kata ya Vingunguti hasa shule ya Msingi Kombo kiwango cha taaluma kitapanda   ufaulu ongezeka zaidi.

Aliwataka wadau wengine kuisaidia sekta katika kuunga mkono juhudi za Rais John Magufuli Mpango wa elimu bure.

Kwa upande wake Ofisa Mahusiano kwa Umma Sereri Nyangita kutoka Taasisi ya PMM  alisema PMM inashughulika na shughuli mbalimbali za Kikamii ikiwemo masuala  ya sekta ya elimu.

Sereri alisema kampuni yao ya PMM ni Wawekezaji katika Wilaya ya Ilala kata ya Vingunguti wamesaidia na serikali katika shughuli za kijamii ikiwemo masuala ya elimu.

Alisema katika kata hiyo ya Vingunguti wanasaidiana na serikali katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili eneo hilo ikiwemo uboreshaji wa miundombinu ya barabara.

Alisema PMM inaunga mkono  serikali  ya awamu ya tano katika kumsaidia Rais John Magufuli.

Naye Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kombo Stella Muhando alipongeza msaada huo uliotolewa na Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto.

Mwalimu Stella alisema shule hiyo imekuwa ikifanya vizuri mwaka hadi mwaka kitaaluma  wanafunzi wanashika alama nzuri.

Akielezea idadi ya Wanafunzi wa shule hiyo alisema Wanafunzi wapo 3000 na Idadi ya Walimu 32  kati yao Wanaume 5 wanawake 32.

Mwisho
Share To:

msumbanews

Post A Comment: