Mwanasheria wa Chama cha Wanasheria Mkoani Tanga (Tawla) Mwanaidi Kombo akisisitiza jambo wakati wa mafunzo ya sheria katika masuala ya ardhi na jinsia kwa Jukwaa la Wanawake mkoani Tanga yaliyoandaliwa na chama hicho

 Mratibu wa Chama cha Wanasheria Wanawake Mkoani Tanga Wakili Latifa Ayoub akizungumza wakati wa wa mafunzo ya sheria katika masuala ya ardhi na jinsia kwa Jukwaa la Wanawake mkoani Tanga yaliyoandaliwa na chama hicho
 Mshiriki wa mafunzo hayo kutoka Kisiwani wilayani Muheza Mwansiti Bashiru akizungumza wakati wa mafunzo hayo
 Washiriki wakiwa kwenye mafunzo hayo

Washiriki wakiwa kwenye mafunzo hayo wakimsikiliza muwezeshaji.
 Washiriki wakipata picha ya pamoja mara baada ya kumalizika mafunzo hayo

MFUMO dume, mila kandamizi kwa wanawake kwenye kumiliki ardhi vimetajwa kuchangia kwa asilimia kubwa upotevu wa haki zao katika jamii zinazowazunguka.

Hayo yalisemwa na Mwanasheria wa Chama cha Wanasheria Mkoani Tanga (Tawla) Mwanaidi Kombo wakati wa mafunzo ya sheria katika masuala ya ardhi na jinsia kwa Jukwaa la Wanawake mkoani Tanga.

Alisema vikwazo vingine ni mila za kibaguzi kwa wanawake ambazo zimechangia kwa asilimia kubwa upotevu wa haki za wanawake hasa kwenye kumiliki ardhi na kujikuta wakishindwa kupata haki yao ya msingi.

“Kwa kuliona hili na ndio maana sisi kama Tawla kumeamua kutoa mafunzo ya kuongezea uelewa Jukwaa la Wanawake mkoani Tanga kwa lengo la kuweza kutambua haki zao na namna ya kuweza kuzidai inapotokea “Alisema

Alisema licha ya hivyo lakini pia wameamua kuanza kutoa elimu kwa kundi la wanawake ikiwemo kuanzisha klabu mbalimbali za mashuleni lengo likiwa ni kuwaoa elimu wanafunzi ili waweze kujua haki na kuweza kupunguza ubaguzi kwenye jamii.

Awali akizumza mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo Mkazi wa Bweni wilayani Pangani Mwajuma Ally alisema wanashukuru kupata elimu hiyo ambayo imewafungua kuweza kutambua haki zao na namna ya kuweza kuzidai kwa kutumia sheria.

Mwajuma alisema awali walikuwa hawatambua wapi wanaweza kwenda kudai haki zao wakati wanapokumbana na changamoto kwenye ndoa hususani yanapokuwa yakijitokeza matatizo mbalimbali.

Mafunzo hayo ya siku mbili yamewashirikisha washiriki kutoka wilaya za Pangani, Tanga na Muheza ambao kwa pamoja wanapewa elimu katika masuala ya ardhi na jinsia kwa Jukwaa la Wanawake.

Mwisho.
Share To:

Post A Comment: