Polisi
mkoani Tanga wamewaua watu watano wanaodhaniwa kuwa ni majambazi
waliotaka kuvamia na kupora mishahara ya wafanyakazi katika shamba la
mkonge la Toronto wilayani Korogwe mkoani Tanga.
Tukio
hilo lilitokea usiku wa kuamkia leo Jumatatu saa 2:00 usiku kwenye eneo
hilo ambako majambazi hayo yaligundua siku hiyo wafanyakazi wangelipwa
mishahara yalikwenda kuvamia na kutaka kupora fedha hizo.
Katika
tukio hilo, mkuu wa upepelezi wilaya ya Korogwe, Samson Mwandambo,
alipigwa risasi kufuani lakini kwa sababu alikuwa amevaa koti la kuzuia
risasi (buleti Proof ) lilimsaidia risasi kutopenya hadi mwilini mwake.
Akizungumzia
tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoani Tanga, Edward Bukombe, amesema
baada ya askari kupata taarifa hizo walifuatilia na majambazi hayo
yalipoona hali hiyo yalianza kurushiana risasi na askari kwa saa kadhaa.
Akielezea
namna tukio hilo lilivyokuwa, Bukombe amesema majambazi hayo yalianza
mapambano na askari kuanzia eneo la Mombo mpaka eneo la Toronto wilayani
hapa.
Amesema katika majibizano hayo ya risasi, polisi waliwapiga risasi majambazi hayo na kuwadhibiti.
Kamanda
huyo amesema baada ya kumalizika kwa majibizano hayo ya risasi, polisi
waliyaua majambazi hayo na kukuta bunduki mbili aina ya Shotgun kwenye
eneo la tukio na bastola ambazo zilikuwa na risasi tano na maganda
matatu ya risasi ambayo walirushiana na askari eneo hilo.
Amesema miili ya majambazi hao imehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Korogwe, Magunga, kwa ajili ya taratibu nyengine.
Post A Comment: