Waziri wa katiba na sheria Balozi Dr Augostine Mahiga amewataka wahudumu wa taasisi zinazo toa huduma za msaada wa kisheria nchini kuongeza juhudi katika utoaji elimu za masuala ya kisheria ili kuweza kupunguza baadhi ya migogoro katika jamii.
Akiwa jijini arusha katika kongamano maalumu la watoa huduma za msaada wa kisheria amesema serikali imekuwa ikishirikiana na shirika la UNDP katika kuhakikisha wananchi wanasaidika katika masuala ya kisheria licha ya changamoto mbalimbali zilizo ndani ya jamii kutokana na ukosefu wa elimu ya masuala ya kisheria.
“Watoa huduma wengi nchini wamekuwa wakifanya huduma hii katika muktadha wa kiharakati suala ambalo si vyema kwa maslahi ya wananchi wanyonge wasio jiweza” alisema Mahiga.
Bi. Christina Kamili ni msajili wa taasisi za utoaji huduma za msaada wa kisheria anasema ipo haja ya kuzingatia kanunia na masharti ya utoaji huduma kutokana na baadhi ya taasisi kukiuka taratibu na kufanya shughuli zao kwa miongozo isiyo halali ambapo anatumia kongamano hilo kusisitiza ueledi na uwajibikaji kwa maslahi mapana ya wananchi wa Tanzania wenye kuhitaji huduma.
Cheles mahole ni miongoni mwa washiriki wa kongamano hilo anaeleza baadhi ya changamoto katika harakati za utoaji huduma kwa wananchi ambapo amesema katika maeneo ya nje ya miji bado suala la mila imekuwa tatizo kubwa na kupelekea migogoro mingi katika familia.
“elimu bado inahitajika ili jamii iweze kuelewa namna ya kujitetea katika mihimili ya kisheria na kuondokana na uwoga pamoja na matendo hasi” alisiema.
Kwa upande wake naibu katibu mkuu wizara ya katiba na sheria Amon Mpanju amenesema ni wakati muafaka kwa watoa huduma za misaada ya kisheria kuzingatia maadili ya kazi zao husasani katika kipindi kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na changuzi nyengine ndogo.
Suala la ukosefu wa elimu na msaada wa kisheria imekuwa likiwaathiri zaidi wakina mama wajane na watoto kutokana na umbali,mazingira yasiyo rafiki juu ya namna ya kuwafikia baadhi ya wananchi katika baadhi ya maeneo kutokana na sababu za kijografia.
Post A Comment: