KATIBU
Mkuu wa CCM Dkt.Bashiru Ally Kakurwa akizungumza katika Kipindi Maalum
kinachozungumzia Kumbukumbu ya Siku ya Mashujaa Zanzibar huko katika
Kituo cha Radio ya Bahari FM Migombani Zanzibar.
RAIS
mstaafu wa Zanzibar wa awamu ya Sita Dkt.Amani Abeid Karume(kushoto),
Katibu Mkuu wa CCM Dkt.Bashiru Ally Kakurwa(katikati) na Naibu Katibu
Mkuu wa CCM zanzibar Dk.Abdulla Juma mabodi(kulia).
KATIBU Mkuu wa CCM Dkt.Bashiru Ally Kakurwa(kushoto),Mke wa Rais wa
kwanza wa Zanzibar Mama Fatma Karume(katikati),Naibu Katibu Mkuu wa CCM
zanzibar Dk.Abdulla Juma mabodi(kulia)wakiwa na Mama Fatma Karume
nyumbani kwake Maisara.
Naibu
Katibu Mkuu wa CCM zanzibar Dk.Abdulla Juma mabodi(kushoto)
akibadilishana mawazo na Katibu Mkuu wa CCM Dkt.Bashiru Ally
Kakurwa(kulia) wakiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hayati Abeid
Karume Zanzibar mara baada ya Katibu Mkuu kuhitimisha ziara yake fupi
iliyoambatana na shughuli ya Hitma ya Siku ya Mashujaa.(PICHA NA IS-HAKA
OMAR-AFISI KUU CCM Z'BAR).
NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.
KATIBU
Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM),Dk.Bashiru Ali Kakurwa amewataka
vijana nchini kuwa mstari wa mbele kulinda kwa vitendo urithi wa fikra
za kimaendeleo zilizoasisiwa na Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi Hayati Sheikh
Abeid Amani Karume.
Alisema
kundi hilo la vijana linatakiwa kujengewa mazingira rafiki ya kuelezwa
na kurithishwa maadili,historia na itikadi yakinifu zinazotokana na
harakati za miongozo ya ASP na TANU ili kupata viongozi bora na makini
wa sasa kama akina hayati Karume,Nyerere na Aboud Jumbe.
Wito
huo ameutoa katika Mahojiano Maalum na Kituo cha Radio ya Bahari FM
kilichopo Migombani Zanzibar, wakati akizungumzia siku ya Mashujaa ya
kumbukizi ya miaka 47 toka kuuawa kwa Rais wa Kwanza wa Zanzibar
Marehemu Mzee Abeid Karume.
Alisema
bila Waasisi wa Mapinduzi ya Januari 12,mwaka 1964 wakiongozwa na
Hayati Karume pasingekuwepo na Muungano pamoja na uhuru wa Waafrika wa
Zanzibar.
Alieleza
kuwa ukweli ni kwamba Mapinduzi hayo ndio chimbuko la uhuru wa kimwili
na kifikra,utu,haki za binadamu,ustawi wa kijamii na kimaendeleo pamoja
na ukuaji wa Demokrasia.
Alisema
miaka 47 ni umri ni mingi lakini ni muhimu kukumbushana kuwa bila jasho
na damu za wanamapinduzi bado Zanzibar mpaka leo ingendelea kuwa chini
ya Utawala wa Kisultani.
"
Lazima tukumbushane japo kwa muda mdogo kwani miaka 47 ni mingi kwa
umri lakini kwa nchi ambayo ni tegemezi na ipo katika nchi zinazoendelea
ni michache sana kwani Watu waliopinduliwa bado wapo na wanatamani
kurudi tena, jambo ambalo haliwezekani.",alisema Dkt.Bashiru.
Pamoja
na hayo alisisitiza mambo matatu ya msingi yanayotakiwa kuzingatiwa na
Vijana pamoja na makada wa CCM kuwa kwanza kutambua historia halisi ya
Taifa lao, pili kusimamia misingi ya waasisi wa Taifa lao na tatu kuwa
wabunifu ili waendeleze mapambano katika Mazingira Mapya ya zama za sasa
za Sayansi na Teknolojia.
Dkt.Bashiru
aliweka wazi kuwa ukombozi haupatikani bila ya mapambano baina ya pande
mbili, hivyo CCM katika suala la Mapinduzi na Muungano ni lazima iwe
imara katika kulinda upande wa kulinda historia isipotoshwe na
waliopinduliwa.
Alisema
CCM ambayo imeshinda kwa awamu ya kwanza ya ukombozi wa kisiasa ni
lazima Jeshi lake ambalo ni Wanachama, Viongozi na Watendaji wasibweteke
bali waendelee kuongeza nguvu za kumiliki umma na kuhakikisha upinzani
unakosa sifa za kubaki katika ushindani wa kisiasa.
"Tusipojiimarisha
vizuri hata haya Mapinduzi tunayoyazungumzia leo yatatuponyoka kwani
mifano ipo mingi Nchi kama Somalia, na Sudan yaliwahi kuwa Mataifa huru
yakawa shwari lakini leo hii katika mataifa hayo kunawaka
moto.",alifafanua Katibu Mkuu huyo.
Aliongeza
kuwa uwepo wa Muungano ni kwa sababu unalindwa hivyo ni muhimu
kuambizana ukweli kuwa waliopinduliwa bado wapo na hawautaki muungano na
wanaendelea kujenga hoja dhaifu ili muungano huo uvunjike.
Akizungumzia
dhana ya Umoja uliossisitizwa na Waasisi wa Mapinduzi Dkt.Bashiru
alieleza kuwa dhana hiyo ya umoja inatakiwa kurutubishwa hasa katika
kusimamia misingi ya ukweli,haki,usawa na utu.
Katika
maelezo yake Dkt.Bashiru alifafanua kuwa pindi wananchi wanapoanza
kudharau yale yaliyopatikana kwa jasho na damu basi panavunjwa msingi
mkuu wa maendeleo.
Alisema
watu wanatakiwa kupewa haki mbali mbali kama haki ya kufikri, haki ya
elimu, haki ya Afya pamoja na haki ya elimu pamoja na haki ya kujitawala
kama Taifa mambo ambayo toka enzi ya Katiba za ASP na TANU mpaka hivi
sasa zimeanishwa vizuri katika Katiba ya CCM ya mwaka 1977 iliyoeleza
namna ya haki kuzilinda na kuzisimamia haki hizo.
Alisema
CCM na Serikali zake inapambana vikali na vitendo vya rushwa ambayo
ndio chimbuko la kuwakosesha haki mbali mbali wananchi.
Dkt.Bashiru
akizungumzia mfumo wa Vyama vingi kuwa upo Kikatiba na Kisheria na
kueleza kuwa miongoni mwa faida za mfumo huo ni vyama hivyo kuchangia
uwepo wa amani na utulivu.
Alisema
Chama Cha Mapinduzi hakikukurupuka kukubali mfumo huo bali kiliamini
kuwa vyama hivyo vitakuwa na imani ya kisiasa,kushindanisha imani hizo
na mikakati ili kupata Taifa bora na imara kwa nyanja zote hatua ambayo
bado haijafikiwa.
Pamoja
na hayo alipongeza kasi ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa upande wa
Zanzibar kwa kueleza kuwa ameridhishwa na kazi hiyo ambayo ndio sehemu
muhimu ya Chama Cha Mapinduzi kujijenga kisiasa kwa kuvuna wanachama
wengi.
Aidha
alitoa wito kwa Wanachama wa CCM kwa Zanzibar na Tanzania bara kuwa
wahakikishe CCM inashinda kwa kura nyingi katika Uchaguzi wa Serikali za
Mitaa mwaka 2019 pamoja na uchaguzi Mkuu wa Dola wa mwaka 2020,ili
kuendelea kulinda Tunu za Taifa za Muungano na Mapinduzi ya Zanzibar.
Katika
mahojiano yake hayo aliahidi kuwa CCM itaimarisha Vyombo vyake vyoye
vya Habari vilivyopo Zanzibar na Tanzania bara ili Watendaji wake
wafanye kazi katika mazingira rafiki na kupata maslahi yanayoendana na
hadhi ya Taasisi wanayoifanyia kazi.
Pamoja
na hayo alizipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na CCM kwa
ujumla kwa kuandaa utaratibu mzuri wa kuwaenzi na kuwaombea Dua ya
Kitaifaa Waasisi mbali mbali walioshiriki katika harakati za Ukombozi wa
Zanzibar wakiongozwa na Hayati Karume.
Mapema
Katibu Mkuu huyo aliwatembelea Viongozi wastaafu mbali mbali wa CCM na
Serikali zake akiwemo Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM Zanzibar ambaye
pia ni Waziri wa Zamani wa Mambo ya Ndani wa Serikali ya awamu ya Tatu
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ali Ameir Mohamed, Rais mstaafu wa
awamu ya Sita Dkt. Amani Abeid Karume na Mke wa Rais wa kwanza wa
Zanzibar Mama Fatma Karume
Post A Comment: