Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani, Joketi Mwegelo ameeleza kuwa harambee ya kuchangia ujenzi wa shule ya sekondari ya wasichana wilayani humo imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwani hadi sasa wamefanikiwa kukusanya Tsh. Milioni 915 kati ya Tsh.Bilioni 1.3 ambazo zinahitajika kufanikisha ujenzi huo.
Uchangiaji wa shule hiyo ya sekondari ambayo itajengwa katika Kata ya Kibuta ,ni muendelezo wa kampeni ya tokomeza ziro wilayani Kisarawe iliyoanzishwa na Jokate kwa kushirikiana na viongozi wengine.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mwegelo amesema baada ya kuzindua harambee ya kuchangisha fedha za ujenzi huo wameamua leo kutoa mrejesho kwa Watanzania wa nini ambacho kimepatikana. "Tumefanikiwa kukusanya Sh. milioni 915 kati ya Sh. bilioni 1.3 tulizolenga kukusanya.
Fedha taslimu ambazo zimeshawekwa benki hadi jana ni Sh. milioni 80 na bado tumeendelea kupokea ahadi za wadau mbalimbali wanaotaka kuchagia. " Mbali na michango ya fedha tuliyopokea, Chama cha Wahandisi Wanawake, wamejitokeza kutoa ushauri wa namna ya kujenga mabweni hayo.
Pia amesema wapo wadau waliochangia mabweni mawili yanayochukua wanafunzi 80 kila moja na lengo ni kujenga mabweni sita. DC Jokate amewashukuru wananchi wa Tanzania na wadau wa maendeleo waliojetokeza kuchangia kampeni hiyo ya kuwakomboa watoto wa kike kwa kuwawekea mazingira wezeshi ya kupata elimu, ingawa kwa siku za usoni watajenga na ya watoto wa kiume kwani kupanga ni kuchagua.
Post A Comment: