Aliyekuwa Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari (CHADEMA), amesema anakubaliana na uamuzi wa chama chake wa kutosimamisha mgombea katika jimbo hilo, kwa kuwa kusimamisha mgombea ni sawa na kubariki uovu na uonevu kwa wananchi.
Tayari Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC), imetangaza uchaguzi mdogo wa ubunge Arumeru Mashariki utafanyika Mei 19 mwaka huu.
CHADEMA kupitia Katibu Mkuu wa chama hicho Dk. Vicent Mashinji walieleza kuwa hawatashiriki uchaguzi huo kwa kile alichodai ni kupoteza muda.
Utakumbuka Machi 14, 2019 Spika wa Bunge Job Ndugai, alitangaza kumvua Nassari ubunge wa jimbo la Arumeru Mashariki kwa makosa ya mahudhurio hafifu bungeni ikiwemo kukosa vikao vya mikutano mitatu ya Bunge.
Post A Comment: