Dr. Rugemeleza Albert Kamuhabwa Nshala amechaguliwa kuwa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), katika uchaguzi uliofanyika jana jijini Arusha, baada ya kupata kura 629 kati ya 1,162. Dkt Nshala alikuwa Makamu wa Rais wa TLS katika uongozi.

Kura za Urais:

1. Dr. Nshala - 629
2. Ngwilimi - 323
3. Wasonga - 123
4. Mwananyela - 58
5. Seka - 29

Sasa ni rasmi kuwa Albert Kamuhabwa Nshala anachukua nafasi ya Mwanasheria Fatma Karume anayeelekea kumaliza muda wake. Fatma alichukua kijiti hicho wa uongozi kutoka kwa Tindu Lissu ambaye hakufanikiwa kumaliza muda wake wa uongozi kutokana na kushambuliwa kwa risasi.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: