Halmashauri zote nchini zimetakiwa kutokubomoa nyumba za wananchi ambazo zipo kwenye makazi holela,ambayo hayakupimwa na badala yake ziweke utaratibu utakaowezesha kuwapatia hati miliki wa nyumba hizo.
Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Ardhi, nyumba na makazi, William Lukuvi ,alipokuwa kwenye maazimisho ya siku ya nyumba Duniani, ambayo imeandaliwa na benki ya NMB, kwa lengo la kuhamasisha wananchi kuchangamkia fursa ya mikopo ya nymba inayotolewa na benki ya NMB.
Waziri Lukuvi,amesema serikali inatambua asilimia 70 % ya wananchi wanaishi kwenye makazi holela ambayo hayakupangwa hawatakiwi kubomolewa nyumba zao badala yake imeaanzisha mpango wa kurasimisha makazi yao na hivyo wasibomolewe nyumba zao.
Amesema serikali katika kuhakikisha wananchi waisho kwenye makazi holela hawabomolewi nyumba zao imewezesha wamiliki wa nyumba hizo ambazo hazikupimwa wapate mikopo ya pesa kutoka kwenye benki ili wajinyanyue kiuchumi.
Lukuvi,amewataka wananchi kuwa wazalendo kwa kupima ardhi zao na kulipia kodi ya serikali ambayo imepunguzwa kutoka asilimia 15% hadi kubakia asilimia 1 % tu na kuhakikisha kila anayejenga nyumba anapata hati miliki .
Post A Comment: