Mkuu wa Mkoa wa MOROGORO DKT.Kebwe Stephen Kebwe ametoa siku kumi na mbili kwa mkurugenzi  Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya MOROGORO ndugu LIYOBA KAYOMBO kukamilisha ujenzi wa majengo ya kituo cha afya cha Mkuyuni.

Dkt
Kebwe ametoa maagizo hayo jana Aprili 8 akiwa katika ziara ya kutembelea shughuli za maendeleo Wilayani humo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Vituo vya Afya Mkuyuni, Duthumi na Hospitali ya Wilaya hiyo.

Dkt. Kebwe amesema kwa muda mrefu amekuwa akifuatilia ujenzi huo pasipo kumridhisha kwa ķuwa mara zote umekuwa wa kusuasua.

Kufuatia hali hiyo Mkuu wa Mkoa analazimika kutoa muda wa kikomo kukamilisha ujenzi huo na kwamba ifikapo Aprili 20 mwaka huu ujenzi wa majengo ya kituo cha Afya Mkuyuni uwe umekamilika tofauti na utekelezaji wa agizo hilo hatua zaidi dhidi yake zitachukuliwa.

Akitetea hali ya kusuasua kwa ujenzi huo Riyoba amesema Changamoto iliyopelekea ujenzi huo kusuasaua ni usimamizi ambao haukuwa thabiti kipindi cha nyuma na kwamba kwa usimamizi uliopo na kwa kasi ya ujenzi uliopo kufikia Aprili 20 ujenzi huo utakuwa umekamilika.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: