Mkuu wa Wilaya ya Arumeru akizungumza wakati wa uzinduzi wa upandaji Miti.

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru akizungumza wakati wa uzinduzi wa upandaji Miti.
Wananchi wa Kata ya Ambureni wakati wa uzinduzi wa siku ya upandaji Miti.

Afisa Maliasili Halmashauri ya Meru ,Charles Mungure akisoma taarifa ya upandaji Miti.
Wadau wa Mazingira na wananchi wakati wa uzinduzi wa siku ya upandaji miti.
Mkazi wa  Shangarai,Ndg.Komba akiyoa maoni .
Afisa Mtendaji wa Kata ya Ambureni  (kulia) akiwa na mtendaji wa Kijiji cha Shangarai.
Wananchi wa Kata ya Ambureni .

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru ,Mhe.Jerry Muro akipanda Mti.
Mkurugenzi  Mtendaji wa Halmashauri ya Meru, Ndg. Emmanuel Mkongo akipanda mti.
Mhe.Diwani wa Kata ya Ambureni Jackson Japhet akipanda mti.
Wananchi Wakipanda Miti.
 
Wananchi baada ya kugawia miche 600 kwaajili ya kupanda majumbani.

Mkuu wa wilaya ya Arumeru, Mhe.Jerry Muro amewataka Watendaji wa Vijiji ,Wenyeviti wa vijiji na Vitongoji  kuwachukulia hatua watu wote watakao bainika kuharibu mazingira kwa kukata  miti ovyo  na kufanya shughuli za kibinadamu kwenye vyanzo vya maji .
Mhe.Muro Ameelekeza hayo wakati maadhimisho ya siku ya upandaji Miti Wilayani humo,yaliyo fanyika  kwa kupanda Miti kwenye chanzo cha Maji Ngololo kilichopo Kata ya Ambureni ,kijiji cha Shangarai.
Akisoma Taarifa ya upandaji Miti katika Halmashauri ya Meru, Afisa Maliasili Ndg.Charles Mungure, amesema mwaka  huu 2018/2019 upandaji miti  unaendelea ambapo jumla ya  miche 587,000 imeshapandwa.
Mungure ameeleza kuwa   upandaji miti kwa mwaka uliopita 2017/2018 unamafanikio makubwa  kwani asilimia 95% ya miche iliopandwa  imepona na  inaendelea vizuri.
Nae Mhe.Diwani wa Kata hiyo Japhet Jackson ameomba uongozi wa Wilaya kudhibiti uharibifu wa mto Nduruma  unaofanywa na wananchi wa Halmashauri zinazopakana na kata hiyo.
Wananchi wa Shangarai wametoa wito kwa wanchi wenzao wa vijiji vingine 4 wanaotegemea chanzo cha maji Ngololo, kukitunza "tutaendelea  kutunza chanzo hichi kwani tumejenga uzio uliogharimu milioni tisa " amesema Komba mwanakijiji wa kijiji cha Shangarai
Aidha katika Hafla hiyo miche 600 imetolewa  kwa wananchi kupanda majumbani .
Share To:

msumbanews

Post A Comment: