NA HERI SHAABAN
MKUU wa Wilaya ya Ilala SOPHIA MJEMA leo amezindua Kamati ya Amani ya Wilaya ya Wilaya Ilala
Alisema viongozi ambao wanachaguliwa katika Kamati hiyo nataka mfanye kazi za Wananchi kwa dhumuni la kuisaidia serikali ya awamu ya tano.
Aidha alisema anajua kamati ya Amani Wilaya ya Ilala itakuwa na majukumu mengi katika kuisaidia serikali ya Rais John Magufuli na kazi kubwa watakayofanya Kamati hiyo kushiriki pia na Kamati ya Ulinzi ya Wilaya.
''Naomba Kamati hii ambayo nimezindua leo ifanye kazi Kwa ushirikiano na kudumisha umoja
Rais John Magufuli ameweka utaratibu wa kukutana na Viongozi wa dini sisi kama Wilaya ya Ilala utaratibu wetu tutakuwa tunakutana na Kamati ya Amani ambayo ndani yake ina viongozi wa dini pia "alisema.
Mjema aliwataka wananchi wa wilaya hiyo kudumisha amani na mshikamano ili kuleta maendeleo katika wilaya ya Ilala na Serikali kwa ujumla.
Awali Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala SHEILA EDWARD alisema kamati hiyo inaundwa wajumbe mbalimbali wakiwemo, viongozi wa dini, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Katibu,Mwenyekiti,Mweka Hazina, Makamu Mwenyekiti, Kaimu Katibu na Wanawake wanne Waislamu wawili na Wakristo wawili.
Kwa upande wake Sheikhe wa Wilaya ya Ilala Adamu Mwinyipingu alisema Kamati ya Amani ni chombo Muhimu sana katika kuimalisha ulinzi.
Sheikh Adam alisema watafanya kazi kwa ushirikiano katika kuisaidia serikali katika kudumisha Amani.
Mwisho
Post A Comment: