Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga Godwin Gondwe ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Handeni akishiriki mbio za kilomita 21 wakati wa mashindano ya Riadha ya Tanga City Marathon Jijini tanga leo |
Washiriki wa mbio hizo kutoka Jijini Tanga wakifurahia medali zao |
KAIMU Mkuu wa Mkoa wa Tanga Godwin Gondwe amesema mkoa huo utaendelea kutumia mashindano ya riadha ya Tanga City Marthon kuweza kutangaza fursa za uwekezaji na utalii zilizopo mkoani Tanga.
Gondwe aliyasema hayo leo wakati akifunga mashindano ya Tanga City Marathon yaliyofanyika jijini Tanga ambapo msimu huu yameshirikisha washiriki 1300 kutoka mikoa mbalimbali na nje ya nchi.
Alisema watafanya hivyo kutokana na kwamba mkoa huo kuwa na maeneo makubwa ya uwekezaji yaliyopo mkoani Tanga ili kuweza kuwa vutia kuwekeza kutokana na fursa kubwa zilizopo.
“Ndugu zangu tutaendelea kuitumia Tanga City marathon kuweza kutangaza mkoa wa Tanga..Lakini pia kutangaza utalii hata uwekezaji mkoa wa Tanga kwani tuna fursa nyingi sana ambazo mnaweza kuzichangamkia kwenye kufanya uwekezaji “Alisema.
Hata hivyo aliwapongeza washiriki ambao wamefanya vizuri kwenye mashindano hayo na kuwataka kuendelea kujiweka imara kwa kushiriki kwenye mazoezi mara kwa mara ili kuweza kujiandaa na yale yajayo.
“Mashindano hayo ya Tanga City Marathon yameufanya mkoa wetu uweze kuendelea kutangazika lakini niwaambie waandaaji wafungue mapema dirisha la usajili msimu ujao “Alisema.
Alisema kwani iwapo watafungua mapema dirisha la usajili wanaweza kupata wadhamini ambao wataweza kuongeza chachu kwenye mashindano hayo msimu ujao.
“Pia niwaambie kwamba Mkuu wetu wa Mkoa Martine Shigella anatambua anatambua sana mchango wenu mlijitokeza kushiriki mashindano hayo na sio kwenye michezo pekee anathamini Tanga City marathon lakini kubwa amenielezea amefurahi kusikia vijana wa shule zetu wameshiriki nao Tanga City Marathon”Alisema.
Hata hivyo pia aliwaagiza wakuu wa shule za Sekondari, Msingi na Vyuo vikuu kuhakikisha wanajiandaa kikamilifu ili kuweza kujipanga kwa ajili ya mashindano yajayo ili nao waweze kupeleka washiriki ambao watashindano kwenye mbio za kilomita tano.
Mwisho.
Post A Comment: