Na Imma Msumba Arusha
Balozi wa Japan nchini Tanzania Shinichi Goto amezindua kumkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe Jerry Cornel Muro kituo cha Afya cha Manyire kilichopo katika kijiji cha Manyere kata ya Mlangarini wilayani Arumeru ambacho kinachotarajia kuhudumia wananchi zaidi ya elfu 10,000 wa kata hiyo na kata za jirani .
Akizungumza katika uzinduzi wa kituo hicho Balozi huyo amesema kuwa serikali ya Japan itaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania katika maendeleo hususan sekta ya afya na miradi ya maendeleo ya jamii.
Amesema kuwa kukamilika kwa mradi huo kutasaidia kuwahudumia wananchi hasa waishio maeneo ya vijijini kwa kusugeza karibu huduma za Afya.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Ndugu Jerry Muro ameipongeza serikali ya Japan na kuiomba kuendelea kushirikiana na serikali hususani katika miradi ya fya jambo ambalo litasaidia kupunguza vifo vya mama na mtoto.
Mbunge wa Arumeru Magharibi Gibson Mesiyaki na Mbunge wa Viti maalumu Amina Molel amesema kuwa kituo hicho cha Afya kitawasaidia wananchi wa kata hiyo pamoja na kinamama wajawazito kuweza kuwa na uzazi salama .
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha Wilson Mahera amesema kuwa kituo hicho kimegharimu kiasi cha shilingi milioni 400 ikiwa na fedha kutoka kwa wahisani pamoja na halmashauri na itakua na manufaa makubwa hususan kwa kinamama .
Matukio mbalimbali katika Picha
Post A Comment: