MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake wa
Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT) Gaudensia Kabaka akikagua bidhaa
zinazotengenezwa na Akina Mama wa Kanisa la Anglicana huko Mbweni
Zanzibar.
WANAWAKE wa Kanisa la Anglicana
wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndugu Gaudensia Kabaka
aliyefika katika Kanisa hilo kwa ajili ya kuwasalimia Akina Mama hao na
kukagua vikundi vya ujasiriamali.
MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake wa
Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT) Gaudensia Kabaka akivishwa sikafu na
Vijana wa Kikundi Maalum cha UVCCM Wilaya ya Dimani Kichama Unguja mara
baada ya kuwasili katika Afisi za Wilaya hiyo kwa ajili ya ziara.
WANAWAKE wa UWT wakiwa Katika
ukumbi wa Afisi ya UWT Kiembesamaki wakimsikiliza kwa makini
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT)
Gaudensia Kabaka katika Kikao cha ndani.
MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake wa
Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT) Gaudensia Kabaka akimkabidhi kadi ya
UWT Mwanachama mpya wa Umoja huo huko Afisi ya UWT Dimani.
……………………….
NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.
MWENYEKITI wa Umoja wa
Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania(UWT), Ndugu Gaudensia Kabaka
amewataka Akina Mama katika Wilaya ya Dimani kicha Unguja kufanya
maandalizi ya kina ya kisiasa yatakayoleta ushindi wa CCM mwaka 2020.
Rai hiyo aliitoa katika
ziara yake wakati akiwahutubia Akina Mama wa UWT wa Wilaya hiyo katika
Afisi za Umoja huo huko Kiembe Samaki Zanzibar.
Alisema Akina Mama
wanatakiwa kujipanga vyema kwa kuhakikisha CCM inashinda na kuendelea
kuongoza Dola katika Uchaguzi Mkuu ujao.
Alieleza kwamba tayari
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM
kwa asilimia 97 hivyo kazi iliyobaki, kwa akina Mama hao ni kunadi,
kutangaza na kueneza Sera za maendelezo zinazotekeleza na Chama pamoja
na Serikali.
Alieleza kuwa maendeleo
yaliyopatikana kwa CCM yamechangiwa na busara na nguvu za Akina Mama
kwani wameanza harakati za kupigania uhuru na maendeleo ya Nchi toka
enzi za ASP na TANU toka Uongozi wa Marehemu Mzee Abeid Karume na Hayati
Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere.
Aliwambia kuwa ni lazima
wanawake waliende hadhi na heshima zao katika kusimamia ukweli na
Falsafa za za Uongozi bora zilizoasisiwa na Akina Mama waasisi wa UWT
toka ilivyoanzishwa.
Alisema kuwa pamoja na
majukumu waliyokuwa nayo katika Medali za Kisiasa ni lazima waendeleze
ubunifu katika kufanikisha kwa vitendo Sera ya Siasa na Uchumi Nchini,
kwa kufanya ujasiriamali ili wajiongezee kipato.
Akizungumza na Akina Mama wa Kanisa la Anglicana huko Mbweni aliwapongeza kwa juhudi zao za kukiunga mkono Chama Cha Mapinduzi.
Aliwambia kuwa Chama cha
CCM hakina ubaguzi wa kidini kwani kinapokea na kufanya kazi na
wanachama wa dini zote, hatua inayokitofautisha na Vyama vingine
vinavyoanzishwa kwa misingi ya kidini.
Aliwasihi Akina Mama hao
kuendeleza umoja na mshikamano wa kudumu kwa kushirikiana katika
masuala mbali mbali ya kukiimarisha Chama Cha Mapinduzi.
Akizungumza Makamu
Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndungu Thuwaiba Kisasi ameeleza kwamba Akina
Mama hao wa kanisa la Anglicana wamekuwa wanachama waaminifu na
wachapakazi kwa kipindi chote na wenye msimamo usioyumba.
Naye Katibu Mkuu wa UWT
Taifa Mwl. Queen Mlozi aliwataka wazazi na walezi kusimamia malezi ya
Watoto wa Kike ili wapate haki ya Elimu bila vikwazo.
Amesema watoto wa Kike
wasiposaidiwa na kulelewa katika mazingira salama hapatopatikana
wataalamu na viongozi jasiri na wachapakazi nchini hivyo wanastahiki
kulindwa.
Kwa upande wake
Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Magharibi Ndugu Zainab Ali Maulid, alisema
wanawake wa Mkoa huo wamekuwa mabalozi waaminifu wa kulinda na kutetea
maslahi ya CCM kwa vitendo.
Katika risala ya Wilaya
hiyo Akina Mama hao wamesema CCM imeendelea kuwa na mvuto na kupendwa na
wananchi kutokana na Utekelezaji Mzuri wa Ilani ya CCM ya mwaka
2015/2020 inayotekelezwa vyema kwa wananchi wote.
Post A Comment: