Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua Mkutano
Mkuu wa Sita wa Maafisa Elimu wa Mikoa na Halmashauri (REDOA) kwenye
ukumbi wa Chuo cha Mipango jijini Dodoma, Machi 26, 2019. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Mwenyekiti wa Umoja wa Maafisa Elimu wa Mikoa na Halmashauri (REDOA), German Mung'aho baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa Sita wa REDOA kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango jijini Dodoma, Machi 26, 2019. Wa pili kulia ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa Joyce Ndalichako, kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Selemani Jafo na kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
JUMANNE, MACHI 26, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Mwenyekiti wa Umoja wa Maafisa Elimu wa Mikoa na Halmashauri (REDOA), German Mung'aho baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa Sita wa REDOA kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango jijini Dodoma, Machi 26, 2019. Wa pili kulia ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa Joyce Ndalichako, kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Selemani Jafo na kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
*Awaonya Maafisa wanajihusisha na wizi waache mara moja
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa onyo kali
kwa baadhi ya Maafisa Elimu wa Mikoa na Wilaya wanaoshirikiana na
waliamu kujihusisha na wizi, udanganyifu na uvujaji wa mitihani waache
mara moja tabia hiyo na mwenendo huo kwa sababu unalivunjia heshima na
hadhi Taifa.
“Kamati
za Mitihani za Mikoa na Wilaya ziendelee kusimamia sheria, kanuni na
taratibu bila ya woga, upendeleo na tusiyumbishwe na hatua za kinidhamu
na kiutumishi kwa mujibu wa sheria.Hatua ziendelee kuchukuliwa dhidi ya
wote wanaobainika kukiuka sheria, taratibu na miongozo inayotolewa”.
Waziri Mkuu ametoa
onyo hilo leo (Jumanne, Machi 26, 2019) wakati wa ufunguzi wa Mkutano
Mkuu wa Sita wa Umoja wa Maafisa Elimu Mikoa na Wilaya(REDEOA),
uliofanyika kwenye ukumbi wa chuo cha Mipango jijini Dodoma. Kauli mbiu
ya mkutano huo inasema “Elimu Bora Itatufikisha Katika Uchumi wa Kati
Ifikapo 2025”
AmesemaBaraza
la Mitihani la Tanzania (NECTA) ni chombo ambacho kwa muda mrefu
kimejijengea sifa kubwa sana nchini na barani Afrika, ambapo Serikali
imewekeza kiasi kikubwa cha rasilimali ili kukifanya chombo hiko kuwa
imara na cha kisasa.
Waziri
Mkuu amesema hali hiyo imezifanya nchi mbalimbali kuja nchini kujifunza
masuala ya upimaji na uendeshaji wa mitihani. “Nimejulilishwa pia hivi
sasa hapa nchini wapo Viongozi wa Mabaraza ya mitihani kutoka nchi za
Afrika Mashariki”.
Wakati huo huo,
Waziri Mkuu amesema suala la tatizo la nidhamu mbaya ya wanafunzi ni
jukumu la walimu wote, hivyo wanatakiwa watekeleze majukumu yao ya
kufundisha, kulea, kuwaongoza na kuwaendeleza wanafunzi kimwili, kiakili
na kiroho kwa uadilifu na kuzingatia sheria.
Waziri
Mkuu amesema Serikali imesikitishwa sana na matukio ya hivi karibuni ya
athari ya viboko kwa wanafunzi shuleni ikiwemo kuvunjwa mikono, kuachwa
na makovu pamoja na tukio la kifo cha mwanafunzi Sperius Eradius wa
shule ya msingi Kibeta Mkoani Kagera.
“Ninatambua
si kusudio la walimu kuwadhuru wanafunzi lakini tukubaliane kuwa kuna
udhaifu katika utaratibu wa utoaji na usimamizi wa adhabu ya viboko
shuleni. Maafisa Elimu kawakumbusheni walimu wote nchini wazingatie
mwongozo wa kutoa adhabu shuleni chini ya kifungu cha 61 cha sheria ya
Elimu sura 353 pamoja na kanuni zake”.
“Adhabu
ya viboko itatolewa iwapo patatokea utovu mkubwa wa nidhamu au kosa
kubwa litakalofanywa ndani au nje ya shule ambalo litaishushia shule
heshima. Na adhabu hii itatolewa kwa kuzingatia umri, jinsia na afya ya
mwanafunzi. Nina hakika tukisimamia utaratibu, matukio haya yaliyoanza
kuonekana yatakoma”.
Kwa upande wake, Waziri
wa Nchi OR-TAMISEMI, Selemani Jafo amewapongeza maafisa Elimu wa Mikoa
na Wilaya hao kwa sababu wanafanya kazi kubwa ambayo imechangia
kupandisha ufaulu wa kidato cha sita na cha nne nchini. Amewasisitiza
waendelee kufanya kazi kwa bidii.
Naye,
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako
amewataka maafisa hao wawe wanatoa taarifa sahihi kuhusu idadi ya
wanafunzi kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya kufundishia na
kujifunzia.
Awali,
Mwenyekiti wa REDEOA, Germana Mung’aho amesema umoja wao unatekeleza
majukumu yao ya kusimamia elimu kikamilifu nchini, lengo likiwa ni
kumuunga mkono Rais Dkt. John Magufuli, ambaye anasisitiza watu wafanye
kazi.
Amesema
umoja huo una wanachama zaidi ya 400 na ulianzishwa ili kusimamia
utoaji wa elimu nchini. Katika mkutano huo wanatarajia kujadiliana
changamoto mbalimbali za sera ya elimu na namna ya kuzipatia ufumbuzi.
Kadhalika,
Mwenyekiti huyo ameiomba Serikali iwapatie magari maafisa hao
watakayoyatumia kwa ajili ya kufuatilia maendeleo ya elimu kwenye maeneo
yao ya kazi, ambapo Waziri Mkuu amesema suala hilo linashughulikiwa.
(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
41193 – Dodoma,
Post A Comment: