Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akiwa na Naibu
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Ackson
Mwansasu mara baada ya kuwasili katika eneo la Uyole Jijini Mbeya
kusikiliza na kutatua kero za wakulima wa viazi mviringo, jana tarehe 5
Machi 2019. (Picha Na Mathias Canal, Wizara ya KIlimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akiteta jambo na Naibu
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Ackson
Mwansasu wakati wakiwa katika eneo la Uyole Jijini Mbeya kusikiliza na
kutatua kero za wakulima wa viazi mviringo, jana tarehe 5 Machi 2019.
Baadhi ya wakulima wa viazi mviringo wakifatilia mkutano wa Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akiwa na Naibu
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Ackson
Mwansasu katika eneo la Uyole Jijini Mbeya kusikiliza na kutatua kero za
wakulima hao, jana tarehe 5 Machi 2019.
Naibu
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Ackson
Mwansasu akizungumza kwenye mkutano na wakulima wa viazi mviringo katika
eneo la Uyole Jijini Mbeya, jana tarehe 5 Machi 2019. Mkutano huo
ulihudhuriwa na Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akiwa na Naibu
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Ackson
Mwansasu mara baada ya kuwasili katika eneo la Uyole Jijini Mbeya
kusikiliza na kutatua kero za wakulima wa viazi mviringo, jana tarehe 5
Machi 2019.
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Mbeya
Waziri
wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga kwa pamoja na Naibu Spika wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Mwansasu wamekubaliana kuvalia
njuga kero sugu zinazowakabili wakulima wa viazi mviringo Mkoani Mbeya.
Kero
zinazowakabili wakulima hao ni pamoja na faini zisizo rafiki za
vifungashio, Ufungaji wa mifuko (zipu) wakati wa kusafirisha usumbufu wa
mawakala wa kilimo wakati wa kusafirisha viazi pamoja na sheria ya
vipimo kutokuwa rafiki kwani viazi hutofautiana uzito kutokana na msimu.
Kero
nyingine ni pamoja na Rushwa kwa baadhi ya watumishi wa viwango
hususani katika vituo wakati wa kupima katika vituo vya ukaguzi visivyo
rasmi vilivyopo katika eneo la Makambako, Iringa, Morogoro, Mikese na
Kibaha.
Katika
taarifa iliyosomwa na wakulima hao jana tarehe 5 Machi 2019 mbele ya
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga pamoja na Naibu Spika wa Bunge Dkt
Tulia Ackson wakulima hao waliiomba serikali kutatua changamoto hizo
ambazo kwa muda mrefu zimekuwa kero bila kupatiwa majibu.
Mhe
Hasunga alisema kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais
Dkt John Pombe Magufuli imedhamiria kwa dhati kutatua kero zisizo
rafiki kwa wakulima na watanzania wote.
“Kumekuwa
na malalamiko ya muda mrefu sasa kwenye zao hili muhimu la viazi
mviringo nami niwaahidi kutekeleza kwa haraka kadhia hii inayowasumbua
Alikaririwa Mhe Hasunga
Kadhalika,
aliwaeleza wakulima hao waliojitokeza katika mkutano huo kuwa Wizara
yake imejipanga kuhakikisha kuwa wakulima wote nchini wanasajiliwa ili
kubaini kiwango cha mashamba wanayolima na uwezo wa uzalishaji wa mazao.
Vilevile
alieleza kuwa serikali imeanza mkakati wa kuwa na Bima ya mazao kwani
kufanya hivyo wakulima watakuwa na ahueni pindi yanapotokea majanga
katika mazao wanayolima.
Naye
Naibu Spika wa Bunge Dkt Tulia Ackson amewapongeza wakulima hao wa
viazi mviringo kwa kuwa wavumilivu wakati serikali inatafuta ufumbuzi wa
kadhia hizo zinazowakabili.
Alisema
kuwa wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na Wizara ya Viwanda na Biashara
zitakutana kutatua kadhia hizo ili wakulima mkoani Mbeya na mikoa
mingine nchini waweze kuzalisha na kusafirisha mazao yao pasina kadhia
yoyote.
Post A Comment: