Picha hii siyo ya tukio halisi
Waziri wa Afya wa Tunisia, Abdurrauf esh-Sherif amejiuzulu wadhifa wake baada ya kutokea vifo vya watoto 11 katika hospitali moja ya serikali mjini Tunus.
Katika taarifa ya kwanza iliyotolewa na wizara ya afya inasema vifo vya watoto hao vilisababishwa na ugonjwa wa maambukizi kwenye damu.
Ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu wa nchi hio ilitoa taarifa kwamba inafuatilia kwa ukaribu kesi hiyo na kwamba ikifahamika kuna uzembe wowote ulifanyika, wahusika watachukuliwa hatua kali.
Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Yusuf Esh Shahid baada ya kuitembelea hospitali ya Er Rabita amesema kwamba amepokea na kukubali kujiuzulu kwa waziri wake.
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari vya kimataifa, idadi ya vifo vilivyotokea katika hospitali hiyo ni 11.
Post A Comment: