Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipongezwa na Waziri wa Madini, Dotto Biteko baada ya kufungua Soko la Dhahabu mjini Geita, Machi 17, 2019. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel na kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Geita, Alhaji Said Kalidushi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
WAZIRI
MKUU, Kassim Majaliwa ametoa tahadhari kwa wadau wote wa madini kuwa
atakayekamatwa anatorosha madini, atachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo
utaifishaji wa madini atakayokuwa akiyatorosha.
Pia
amewataka viongozi na watendaji wote wa Serikali wasimamie kwa weledi,
uaminifu na uadilifu, sheria, kanuni na miongozo kuhusu sekta ya madini
kwa lengo la kudhibiti utoroshwaji wa madini hususan dhahabu kwenda nje
ya nchi.
Waziri
Mkuu ametoa tahadhari hiyo leo (Jumapili, Machi 17, 2019) wakati
akifungua soko la madini la Mkoa wa Geita. Ufunguzi wa soko hilo ni
utekelezaji wa agizo la Rais Dkt. John Magufuli alilotoa tarehe
22.01.2019 la kuitaka mikoa yote ianzishe masoko ya madini.
Waziri Mkuu ameitakaWizara
ya Madini, Tume ya Madini, Serikali ya Mkoa, Idara na Taasisi nyingine
za Serikali zinazohusika na maendeleo ya sekta ya madini waheshimu
mipaka ya majukumu yao ili waweze kulisimamia vizuri soko hilo na
kufanya kazi kama ilivyokusudiwa.
“Wizara
ya Madini ishirikiane na vyama na mashirikisho ya wachimbaji na
wafanyabiashara wa madini kuandaa mpango kazi mahsusi kwa ajili ya
utekelezaji wa majukumu ya soko hili ili lisigeuke kuwa kikwazo kipya
kwa wachimbaji na wafanyabishara wa madini”
Waziri Mkuu ameviagizaVyombo
vya Ulinzi na Usalama vihakishe soko hilo linapata ulinzi wa kutosha
muda wote ili watendaji, mali zitakazokuwemo, vitendea kazi na
miundombinu yote iwe salama muda wote. “Mkuu wa mkoa na Wakuu wa vyombo
vya ulinzi na usalama, nawaagiza hakikisheni Suala hili mnaliandalia
utaratibu haraka iwezekanavyo”.
Pia,
Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuielekeza mikoa mingine yenye kiwango
kikubwa cha uzalishaji wa madini hususan ya metali na vito iharakishe
uanzishwaji wa masoko ya madini sanjari na miundombinu yote muhimu ili
masoko hayo yaanze kufanya kazi kabla ya kwisha kwa mwaka huu wa fedha
2018/2019.
Amesema anaamini kwamba, usimamizi
mzuri wa soko hilo na masoko mengine ya madini yanayoendelea kuanzishwa
nchini utaimarisha makusanyo ya kodi za Serikali na kuongeza mchango wa
sekta hiyo kwenye pato la Taifa.
Vilevile,
amesema wafanyabiashara wa madini, hususan kutoka nje ya nchi
wataongezeka kwa sababu tutakuwa tumewaepusha na matapeli na vikwazo
vingine vya kibiashara. “Uimara wa soko hili pia, utaboresha uhusiano
kati ya wadau wa biashara ya madini na Serikali”.
Waziri
Mkuu amesema Serikali imefuta baadhi ya tozo na kodi ambazo zilikuwa
kero kwa wafanyabiashara wa madini hususan wachimbaji wadogo. Miongoni
mwa tozo zilizofutwa ni Kodi
ya Ongezeko la Thamani (VAT) na Kodi ya Zuio ya asilimia tano ya mwisho
(final withholding tax) inayotozwa kwenye bei ya kuuzia madini ya aina
zote.
Amesema
baada ya kufutwa kwa kodi na tozo hizo Serikali inatarajia kuwa
utoroshwaji wa madini utapungua, pia kutasaidia wachimbaji wadogo
kutambuliwa kupitia uanzishwaji wa masoko ya madini; kupunguza gharama
za uendeshaji wa shughuli za wachimbaji wadogo na kuongeza wigo wa
mapato kwa nchi.
“Nitoe
wito kwa wachimbaji wote wadogo kwamba endeleeni kushirikiana na
mamlaka mbalimbali za Serikali katika kutekeleza majukumu yenu kwa
kufuata taratibu, sheria, kanuni na miongozo mbalimbali inayotolewa na
Serikali”.
AmesemaSerikali
inachukua hatua zote hizo si kwa lengo jingine bali kuziba mianya
ambayo imekuwa chanzo cha utoroshwaji wa madini, ukwepaji kodi, na
hivyo, kusababisha biashara nzima ya madini kufanyika kiholela katika
maeneo mengi ya nchi yetu.
Waziri
Mkuu amesema Serikali imejipanga vema katika kuhakikisha vikwazo vyote
vilivyomo katika mnyororo wa biashara ya madini vinaondolewa kwa lengo
la kukuza sekta hiyo na kuwanufaisha wananchi na Taifa kwa ujumla.
Amesema
Serikali imeamua kutoa mwelekeo mpya katika usimamizi na maendeleo ya
sekta ya madini. “Utekelezaji wa dhamira hii unakwenda sambamba na
kuweka mazingira mazuri na miundombinu itakayowezesha kuimarika kwa
sekta ya madini nchini”.
Kadhalika,
Waziri Mkuu amesema wachimbaji wadogo wamekuwa wakilalamikia ukosefu wa
masoko ya uhakika ya madini ambao umekuwa sababu ya utoroshwaji madini,
hivyo kuanzishwa kwa soko hili kunawahakikishia wachimbaji wadogo
masoko na kukua kwa kipato kutokana na shughuli za madini.
Waziri
Mkuu amesema kwa muda mrefu sasa, kumekuwepo na malalamiko ya
kudhulumiwa au kupunjwa kutoka kwa baadhi ya wachimbaji wadogo, vitendo
hivyo vimekuwa vikiwahusisha wafanyabiashara wa madini wasiokuwa
waaminifu.
“Ndugu
wachimbaji wadogo, soko hili linakwenda kuwa mwarobaini wa tatizo hilo
kwani litasheheni vifaa vya kupimia uzito na ubora wa madini kabla
hayajauzwa. Naielekeza Tume ya Madini, isimamie ipasavyo vifaa na
taratibu za vipimo kwenye soko hili na kuhakikisha hakuna manung’uniko
juu ya utendaji kazi wa vifaa hivyo”.
Waziri
Mkuu ameongeza kuwa soko hilo pia litaondoa uwezekano wa wanunuzi wa
madini kuibiwa na wajanja wachache wanaojifanya kuwa na madini wakati
hawana. “Nawasihi wanunuzi wa madini kulitumia soko hili kikamilifu ili
kuepuka udanganyifu na matapeli”.
Pia
ameiagiza Tume ya Madini kuratibu bei za madini ndani ya soko hilo na
ihakikishe mchimbaji anapata stahiki zake, Serikali inapata mapato yake
na mfanyabiashara naye ananufaika. “Tunaimani kabisa tatizo la
kudhulumiana na kupunjana linaenda kwisha kabisa. Na kwa kweli ikitokea
mtu amepunjwa, atakuwa amejitakia mwenyewe”.
“Ndani
ya soko hili kutakuwa na huduma zote muhimu kwa mfanyabiashara ikiwemo
huduma za Tume ya Madini, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mabenki na
nyinginezo, hivyo kuokoa muda na gharama nyingine katika kuendesha
biashara hii ya madini.
Amesema
soko hilo litasaidia sana katika ukusanyaji wa mapato ya Serikali na
takwimu za biashara ya madini. Hivyo, niwasihi wachimbaji wa madini
kulitumia soko hili na kuacha vitendo vya utoroshaji wa madini. Serikali
kwa upande wake, haitomvumilia mtu yeyote yule atakaye jihusisha na
utoroshaji wa madini.
Ufunguzi
huo umehudhuriwa na Waziri wa Madini, Doto Biteko, Waziri wa Nishati
Dkt. Medard Kalemani, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Costantine
Kanyasu, Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila,
Wabunge wa mkoa wa Geita, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robertt
Gabriel, wakuu wa mikoa jirani na maafisa wa Serikali.
(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI, MACHI 17, 2019.
Post A Comment: