Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera,
Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama
akihutubia watumishi wa Ofisi yake walioshiriki katika mkutano wa baraza la
wafanyakazi la ofisi hiyo uliofanyika Machi 18, 2019 katika Ukumbi wa mikutano
wa ofisi hiyo Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala
ya Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki akizungumza jambo wakati wa kikao cha baraza
la wafanyakazi la ofisi hiyo Machi 18, 2019 Jijini Dodoma.Mawaziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Mhe.Jenista Mhagama anayeshughulikia Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu pamoja na waziri anayeshughulikia Uwekezaji Mhe. Angellah Kairuki wakiimba wimbo wa umoja na mshikamano wakati wa mkutano huo.
Sehemu ya wajumbe wa baraza la wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakifuatilia ujumbe kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi hiyo, anayeshughulikia Bunge na Waziri Mkuu Bi.Maimuna Tarishi wakati wa kikao hicho.
Sehemu ya wajumbe wa baraza la wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakifuatilia ujumbe kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi hiyo, anayeshughulikia Bunge na Waziri Mkuu Bi.Maimuna Tarishi wakati wa kikao hicho.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akimkabidhi Katibu mpya wa Baraza la Wafanyakazi wa ofisi hiyo Bw.Pascal Vyagusa nyaraka za utendaji kazi katika nafasi hiyo mara baada ya kuteuliwa na wajumbe wa baraza hilo.
Mkurugenzi wa Sera na Mipango Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Packshard Mkongwa. akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango wa Bajeti ya Ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2018/2019 na Mpango na Makadirio ya Bajeti ya Mwaka 2019/2020 wakati wa kikao hicho.
Mmoja wa wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Amina Simbaulanga akichangia jambo wakati wa kikao hicho.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama pamoja na Waziri wa Nchi ofisi hiyo anayeshughulikia Uwekezaji Mhe. Angella Kairuki wakikata utepe nyaraka za utendaji kazi kwa viongozi wa baraza la wafanyakazi wa ofisi hiyo wakati wa mkutano wa baraza lao.
NA.MWANDISHI
WETU
Watumishi
wa Ofisi ya Waziri Mkuu Uratibu, Sera, Bunge na Uwekezaji wamehimizwa kutumia
muda wao wa kazi kwa umakini katika kutekeleza majukumu yao kwa wakati na
ufanisi wa hali ya juu.
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu,
Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama alipokuwa
akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi cha Ofisi hiyo kilichofanyika Machi
18, 2019 katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi hiyo Jijini Dodoma.
“Ni
wajibu wa kila mtumishi kuzingatia maadili na weledi katika kuhakikisha
utumishi wa umma unaheshimika na kuwajibika kwa ufanisi kwani hakuna haki
pasipo wajibu, hivyo kila mtumishi azingatie hayo ili kuwa na utendaji wenye
manufaa kwa ofisi na Serikali kwa ujumla,”alisema Mhagama
Aidha
Waziri Mhagama ameziagiza mamlaka zinazosimamia nidhamu katika Wizara hiyo
kutosita kuwachukulia hatua za kinidhamu watumishi wasiotimiza wajibu wao katika
maeneo yao ya kazi ikiwemo watumishi wazembe na wenye tabia ya kuchelewa
kazini.
“Serikali
ya Awamu ya Tano ya Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli,inasisitiza utendaji
uliotukuka na bidii kwa kuzingatia adhima ya HAPA KAZI TU, hivyo kila mmoja
ajitathimini kwa kina kuona namna anavyoenenda na endapo akaona kuna kasoro
arekebishe mapema kabla hatua za kinidhamu hazijachukuliwa juu yake,”alisisitiza
Waziri Mhagama.
Naye
Waziri wa Nchi ofisi hiyo anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji Mhe.Angellah
Kairuki alipongeza watumishi wa ofisi hiyo kwa mafanikio yanayoonekana katika
Ofisi hiyo na kutoa wito kwa watumishi kuendeleza jitihada hizo ili kuwa na
mazingira mazuri kwa wawekezaji nchini.
“Kipekee
niwapongeze watumishi wa Ofisi hii kwa kuendelea kutekeleza vizuri majukumu ya
kila siku kwa weledi kwa kuzingatia ukubwa wa ofisi hii, na tuendelee
kutekeleza vya ufanisi ili kuvutia wawekezaji nchini waweze kuona fursa na
kuwekeza,”alieleza Waziri Kairuki.
Kwa upande wake Katibu Mkuu
wa ofisi hiyo anayeshughulikia Bunge na Waziri Mkuu Bi.Maimuna Tarishi alimshukuru mgeni rasmi kwa
kuwafungulia kikao na kuongezea kuwa Ofisi ya waziri Mkuu inapaswa kuwa mfano
katika kusimamia shughuli za mabaraza ikiwa ni sambamaba na kuwataka waajiri
kuendelea kuyathamini mabaraza kwa vitendo kwa kuhakikisha kunakuwa na matokeo
chanya yenye kuimarisha utendaji wa kazi za kila siku.
“Nawaomba
watumishi kuzingatia na kutekeleza wajibu wenu katika majukumu yenu ya kila
siku,kwa kuzingatia kanuni na taratibu zilizoainishwa katika mikataba ya ajira
nasi tunatoa shime kwa waajiri kuendelea
kuzingatia umuhimu wa kuundwa kwa mabaraza haya na kuyatumia kwa usahihi kama
ilivyokusudiwa” asisitiza Bibi.Tarishi
=MWISHO=
Post A Comment: