Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (meza kuu katikati) akiongoza kikao cha Tume ya Jeshi la Polisi, Magereza na Uhamiaji inayoshughulikia masuala ya Kiutumishi na Kiutendaji wa Askari katika Majeshi hayo, katika Ukumbi wa Ofisi ndoo ya Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto Meza Kuu ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhandisi Hamad Masauni. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto) akimuapisha Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali Watu wa Wizara hiyo, Hilda Tegwa kuwa Mjumbe wa Sekretarieti ya Tume ya Utumishi ya Jeshi la Polisi, Magereza na Uhamiaji inayoshughulikia masuala ya Utumishi na Utendaji wa Askari wa Majeshi hayo, katika Ukumbi wa ofisi ndogo ya Wizara hiyo jijini Dar es Salaam leo. Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (meza kuu katikati) akimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali, Jacob Kingu (kulia), alipokuwa anamfafanulia jambo katika kikao cha Tume ya Jeshi la Polisi, Magereza na Uhamiaji inayoshughulikia masuala ya Kiutumishi na Kiutendaji wa Askari katika Majeshi hayo. Kikao hicho kilifanyika, ukumbi wa ofisi ndogo ya Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto Meza Kuu ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhandisi Hamad Masauni. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Post A Comment: