Waziri wa  Nchi Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Seleman Jafo ametoa miezi mitatu  kwa wakurugenzi  wa Halmashauri za Miji, Majiji, Manispaa na Wilaya  nchini kuhakikisha wanatenga asilimia kumi ya mapato ya ndani  kwa ajili ya wanawake, vijana na wenye ulemavu na kutoa mkopo kwa makundi hayo.

Amesema Mkurugenzi atakaeshindwa kutenga asilimia kumi kwaajili ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu atakuwa amekiuka sheria ya Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania kwani suala hilo  lipo kwa mujibu wa sheria.

Waziri Jafo ametoa agizo hilo wakati wa kongamano la vijana  kujadili fursa zilizopo mkoani  Morogoro ambapo amesema ili Tanzania ifikie uchumi wa viwanda  ni lazima kushirikisha makundi maalumu ikiwemo akinamama ,vijana na walemavu kama serikali inavyoagiza, lakini baadhi ya Wakurugenzi wamekuwa wakikaidi kutenga fedha hizo na kuzitumia katika shughuli zingine za maendeleo kinyume na utaratibu

Aidha waziri Jafo ameawataka vijana kutumia fulsa zilizopo katika maeneo yao ili kuondokana na swala zima la ukosefu wa ajiri kwa vijana,ambapo amesma kila eneo kuna fulsa zinazoweza kumpa kijna ajira ikiwemo kilimo na ufugaji.

Katika hatua nyingine, Waziri Jafo ameutaka Ungozi wa Mkoa wa Morogoro kuangalia utaratibu wa  kuufanya Uwanja Wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (eneo la nanenane) kuwa eneo ambalo Wajasiriamali wanafanya kazi zao kila siku tofauti na ilivyo sasa mpaka msimu wa Nanenane.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Kilimo, Omary Mgumba na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Steven wamewataka wakazi wa morogoro kutumia fursa ya viwanda vilivyopo kuzalisha mazao kwa wingi ili kupata soko katika viwanda hivyo.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: