Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo (kushoto) akisalimiana na Binti Mfalme wa Jordan Sarah Zeid wakati wa ziara yake Nchini kukagua miradi ya Lishe inayotekelewa na Shirika la Chakula Duniani (WFP).
Binti Mfalme wa Jordan Sarah Zeid akizungumza na WaziriwaNchi OR- TAMISEMI Mhe. SelemaniJafo (Mb) wakati wa ziara yake nchini kukagua miradi ya Lishe inayotekelewa na Shirika la Chakula Duniani (WFP).
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani
Michael Dunford akizungumza wakati wakikao
1. Waziriwa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo (katikati) akiwa na Binti Mfalme wa
Jordan Sarah Zeid(kushoto) pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la
ChakulaDuniani Michael Dunford
Waziri wa Nchi
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amelitaka
Shirika la ChakulaDuniani (WFP) kuendelea kutoa ushirikiano katika miradi mbalimbali
inayotekelezwa na Serikali ili kuendelea kuboresha masuala ya Lishe katika jamii.
Waziri Jafo ameyasema
hayo wakati wa kikao na Binti Mfalme wa Jordan Sarah Zeid cha kujadili masuala mabalimbali yanayohusiana na Lishe sambamba
na miradi inayofadhiliwa na fedha za Umoja wa Ulaya kupitia Shirika la chakulaDunia.
Waziri Jafo aliwashukuru
kwa ushirikiano wanaowapatia katika miradi mbalimbali ya Lishe na hakika wamekua
na mchango mkubwa katika kuboresha Lishe Tanzania Kwa kuwa Lishe ni suala endelevu
na mtambuka wanaomba wa endelee kutoa msaada zaidi wakifedha na kitaalamu ili Lishe izidi kuboreshwa
katikajamii.
‘HatuwezikufikiaTaifa
la Uchumiwa Kati endapowatuwetuhawatakuwanalishe bora,
iliwatuwafanyakazikwabidii, waweze kuzalisha nakulipa kodi inavyotakiwa nilazima wawe naAfya bora wakati wote hivyo kuendele
akutoa elimunakuhamasishalishe bora
nivitumuhimu sana katika kufikia lengo la Kitaifa” alisema Mhe. Jafo.
Katika kikao
hicho Mhe.Jafo alizungumzia suala la kuanzisha Siku ya Lishe kitaifa itakayoazimishwa
kila mwaka ili kuendelea kutoa Elimu kwa Umma kuhusu umuhimu wa Lishe katika maisha
ya kila siku yamtanzania.
Alimtaka Binti
Mfalme wa Jorda Sarah Zeid kuendelea kutoa ushirikiano katika kufanikisha siku hii
muhimu ya kitaifa itakayoanza kuazimishwa mwaka huu wa 2019.
Naye Binti Mfalme
Sarah Zeid amesema amefurahishwa sana na utekelezaji wa miradi ya Lishe inayotekelezwa katika Halmashauri
nne Nchini na ameridhishwa na matokeo aliyoayaona kuptia miradi ya wananchi.
Ameahidi kupitia
Shirika la Chakula Duniani (WFP) kuendelea kutoa ushirikiano katika miradi mingine
itakayoendelea kutekelezwa ilik uhakikisha Lishe inaboreshwa katika Jamii.
NayeMwakilishi
Mkaazi waShirika la ChakulaDuniani Michael
Dunford amesema watashiriki kikamilifu katika kuadhimisha siku ya Lishe Kitaifa
na watatoa ushirikiano unaohitajika katika kufanikisha siku hiyo.
Shirika la
ChakulaDuniani (WFP) linaratibu mradi wa Boresha Lishe unaotekelezwa katika Halmashauri
nne Nchini ambazo ni Bahi, Ikungi, Singida Dc pamoja na Chamwino.
Post A Comment: