Jengo la Wizara ya Kilimo likiwa katika hatua za mwisho kukamilika katika mji wa serikali Ihumwa Jijini Dodoma. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri
wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya
Kilimo Mhandisi Methew Mtigumwe wakikagua ujenzi wa Ofisi za Wizara
unaendelea kujengwa katika mji wa serikali Ihumwa Jijini Dodoma.
Waziri
wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya
Kilimo Mhandisi Methew Mtigumwe wakikagua ujenzi wa Ofisi za Wizara
unaendelea kujengwa katika mji wa serikali Ihumwa Jijini Dodoma.
Waziri
wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya
Kilimo Mhandisi Methew Mtigumwe wakiwa katika picha ya pamoja na mafundi
wa Ofisi za Wizara katika mji wa serikali Ihumwa Jijini Dodoma.
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Waziri
wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya
Kilimo Mhandisi Methew Mtigumwe kwa kauli moja wameridhishwa na ujenzi
wa Ofisi za Wizara unaendelea kujengwa katika mji wa serikali Ihumwa
Jijini Dodoma.
Mhe
Hasunga amesema kuwa Ofisi hizo zimekamilika kwa asilimia nyingi hivyo
wakati wowote kuanzia hivi sasa watumishi wa Wizara hiyo watapaswa
kuhamia.
Ametoa kauli hiyo mara baada ya kutembelea na kukagua hatua zilizofikiwa za ujenzi wa Ofisi hizo leo Tarehe 14 Machi 2019.
Pamoja
na mambo mengine Waziri Hasunga alimpongeza Rais wa Tanzania Mhe Dkt
John pombe Magufuli kwa uamuzi wake ambao umetoa muelekeo wa serikali
kuwa na mji wake maalumu jambo hilo litaongeza ufanisi katika
kuwahudumia wananchi.
Alisema
kuwa awali maamuzi ya Rais yalipotolewa wengi hawakuelewa makusudi ya
ujenzi wa mji wa kiserikali lakini pindi watumishi wa wizara mbalimbali
watakapohamia katika eneo hilo watabaini umuhimu wake.
Wakati
huo huo Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Methew Mtigumwe
alimueleza Waziri wa Kilimo kuwa ujenzi huo umefikia katika hatua za
mwisho hivyo siku chache zijazo maandalizi ya kuhamia Ihumwa
yatakamilika.
Aliwapongeza mafundi wanaoendelea na ujenzi huo kwa kuwa waaminifu na kukamilisha ujenzi wa majengo hayo kwa wakati muafaka.
Serikali
kuhamia Dodoma ni sehemu ya kukamilisha safari iliyoanza miaka 42
iliyopita ya kuhamishia makao makuu ya Serikali mkoani Dodoma.
MWISHO
Post A Comment: