Waziri
wa Kilimo, Mhe Japhet Hasunga (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na
wadau mbalimbali mara baada ya uzinduzi wa mradi wa kudhibiti Sumukuvu
Tanzania (TANIPAC), ulifanyika katika ukumbi wa Kambarage uliopo katika
jengo la Wizara ya Fedha na Mipango (HAZINA) Jijini Dodoma, Tarehe 12 machi, 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri
wa Kilimo, Mhe Japhet Hasunga (Mb) aakisisitiza jambo wakati akizindua
mradi wa kudhibiti Sumukuvu Tanzania (TANIPAC), ulifanyika katika ukumbi
wa Kambarage uliopo katika jengo la Wizara ya Fedha na Mipango (HAZINA)
Jijini Dodoma, Tarehe 12 machi, 2019.
Waziri
wa Kilimo, Mhe Japhet Hasunga (Mb) akiteta jambo na Naibu Waziri wa
Kilimo Mhe Innocent Bashungwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa
kudhibiti Sumukuvu Tanzania (TANIPAC), ulifanyika katika ukumbi wa
Kambarage uliopo katika jengo la Wizara ya Fedha na Mipango (HAZINA)
Jijini Dodoma, Tarehe 12 machi, 2019.
Katibu
Mkuu wa Wiziri wa Kilimo, Mhandisi Mathew Mtigumwe akitoa maelezo ya
awali kuhusu mradi wa kudhibiti Sumukuvu Tanzania (TANIPAC), ulifanyika
katika ukumbi wa Kambarage uliopo katika jengo la Wizara ya Fedha na
Mipango (HAZINA) Jijini Dodoma, Tarehe 12 machi, 2019.
Waziri
wa Kilimo, Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikata utepe ishara ya uzinduzi wa
mradi wa kudhibiti Sumukuvu Tanzania (TANIPAC), ulifanyika katika ukumbi
wa Kambarage uliopo katika jengo la Wizara ya Fedha na Mipango (HAZINA)
Jijini Dodoma, Tarehe 12 machi, 2019.
Na Mathias canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Watekelezaji
wote wa Mradi wa Kudhibiti Sumukuvu Tanzania- (Tanzania Initiatives for
Preventing Aflatoxin Contamination – TANIPAC) wametakiwa kuhakikisha
kuwa kunakuwa na matokeo chanya katika jamii katika utekelezaji wa mradi
huo ili kuhakikisha kuwa umasikini unapungua (Poverty reduction), na
kujikita kutazama utekelezaji wa matokeo ya kama yatalingana na thamani
ya fedha itakayotumika (Value for Money).
Waziri
wa Kilimo, Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo leo Tarehe 12 machi,
2019 wakati akizindua mradi wa kudhibiti Sumukuvu Tanzania (TANIPAC),
katika ukumbi wa Kambarage uliopo katika jengo la Wizara ya Fedha na
Mipango (HAZINA) Jijini Dodoma.
Alisema kuwa, Mwezi Juni, 2018 Serikali ilizindua Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili au kwa kifupi ASDP II. Programu
ya ASDP II inalenga kuongeza tija katika uzalishaji, kukifanya kilimo
kiwe cha biashara na kuongeza pato la mkulima ili kuboresha maisha,
uhakika wa chakula pamoja na lishe. Program hii inatekelezwa kikamilifu kupitia miradi mbalimbali ili kufikia malengo iliyojiwekea.
Mradi wa TANIPAC unatekelezwa chini ya vipengele (Component) Na. 2 na 3 ambavyo vinalenga kuongeza tija katika uzalishaji na kuongeza thamani ya mazao. Thamani ya mazao ni pamoja na chakula salama ambacho kinaenda kuuzwa kwa walaji ndani na nje ya nchi. Na kwa kuwa ASDP II inalenga kukifanya Kilimo kuwa cha kibiashara, ni dhahiri mazao yanayotakiwa kuuzwa ni yale yaliyo salama.
Alisema, utekelezaji wa mradi huo utasaidia katika kutimiza malengo ya ASDP II ambayo yana Kaulimbiu inayosema: Chakula ni Uhai. Tafsiri
ya Kaulimbiu hii ni: - chakula salama ni msingi wa maisha, hivyo hapana
budi kuimarisha mfumo wa uzalishaji wa chakula salama.
Waziri Hasunga alisema kuwa Suala la kuimarisha biashara
na masoko pamoja na uhakika wa chakula na lishe pia ni vipaumbele
muhimu katika utekelezaji wa mpango wa uwekezaji na usalama wa chakula
katika sekta ya Kilimo (Tanzania Agricultural and Food Security Investment Plan -TAFSIP) na Mpango wa Kuendeleza Sekta ya Kilimo Bara la Afrika (Comprehensive African Agriculture Development Program – CAADP) kama ilivyoelekezwa kwenye Azimio la Malabo.
Kadhalika, suala la usalama wa chakula ni hitaji la lazima katika kufikia Malengo Endelevu ya Dunia (Sustainable Development Goals, SDGs), hususani Lengo Na.2.1, 3.2 na 2.3 ambayo
kwa ujumla yamelenga kukomesha njaa, kuhakikisha kuwa kuna usalama wa
chakula na lishe, kilimo endelevu, kuimarisha afya na siha za watu
nakupunguza upotevu wa chakula kwa kiwango cha asilimia 50 ifikapo mwaka
2030.
“Ili tuweze kuelewana vizuri nataka tutofautishe dhana ya usalama wa chakula (food security) na chakula salama (food safety). Mradi
tunaozindua leo ni wa kuhakikisha chakula tunachozalisha, tunachouza na
tunachokula ni salama kwa maana ya kutokuwa na sumu inayoweza kuathiri
afya za watumiaji. Usalama wa chakula ni hali ya kuwa na
uhakika wa chakula cha kutosha na chenye viini lishe vya kutosha katika
ngazi ya kaya na Taifa” Alikaririwa Mhe Hasunga na kuongeza kuwa
“Ni
muhimu tukafahamu kuwa, suala la chakula salama (food safety) ni tatizo
Duniani kote na huathiri mataifa yote, hasa yale yanayoendelea kama
Tanzania na nchi nyingine za dunia ya tatu. Hii inatokana na kutokuwa na
mifumo imara ya usimamizi katika nyanja za uzalishaji wa chakula,
uhifadhi na ugavi”
Mhe
Hasunga alieleza kuwa Changamoto hiyo ya chakula salama inachangia kwa
kiasi kikubwa kudhoofisha afya za Walaji, wakati mwingine vifo na athari
nyingine nyingi zikiwemo za kiuchumi.
Tatizo
la sumukuvu si geni katika Ukanda wa Afrika Mashariki Kwa mfano, tatizo
hilo limekuwa likijitokeza mara kadhaa katika nchi ya Kenya ambapo
mwaka 2004 watu zaidi ya 300 walipata ugonjwa wa Aflatoxicosis utokanao na sumukuvu na kusababisha vifo vya Watu 125 baada ya kula chakula kilichokuwa na kiwango kikubwa cha sumukuvu.
Tatizo
kama hilo liliwahi kutokea nchini mwaka 2016 ambapo zaidi ya watu 60
katika Halmashauri za Bahi, Chemba, Kiteto na Kondoa waliugua baada ya
kula chakula chenye kiwango kikubwa cha sumukuvu na watu 19 kufariki kwa
tatizo hilo.
Mradi wa TANIPAC ambao umezinduliwa na Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga unalengo la kupunguza sumukuvu (aflatoxin) katika mazao ya mahindi na karanga.
Aidha,
Taarifa zinaonesha kuwa tatizo la Sumukuvu ni kubwa kwani inakadiriwa
kuwa asilimia 25 ya mazao yote yanayozalishwa duniani yanaathiriwa na
Sumukuvu.
Tafiti
za kiafya zinabainisha kwamba, sumukuvu huchangia zaidi ya aina 25 za
saratani na kipekee inachangia asilimia 30 ya saratani ya ini. Pamoja na kuchangia saratani, kuna ushahidi wa kisayansi unaoonesha kwamba sumu hiyo huchangia udumavu kwa watoto ambapo yanaathiri ukuaji wa mtoto kimaumbile pamoja na kuchangia kudumaa kwa akili. Vilevile,
tatizo la sumukuvu huathiri biashara ya mazao ya chakula katika soko la
Kimataifa ambapo kwa Bara la Afrika linapoteza zaidi ya Dola za
Marekani Milioni 670 ambayo ni sawa na asilimia 40 ya mauzo yote ya nje
yanayokataliwa kila mwaka.
Post A Comment: