Waziri wa Madini Doto Biteko
akimsikiliza Rais wa Kampuni ya Amtec Resources Management Ltd ya nchini
Uingereza, Dkt. Peter Gollmer.
Waziri wa Madini Doto Biteko
akizungumza jambo na Rais wa Kampuni ya Amtec Resources Management Ltd
ya nchini Uingereza, Dkt. Peter Gollmer. Anayefuatilia ni Mkurugenzi wa
Ssera na Mipango Wizara ya Madini, Augustine Ollal.
Waziri wa Madini Doto Biteko
akiteta jambo na Rais wa Kampuni ya Amtec Resources Management Ltd ya
nchini Uingereza, Dkt. Peter Gollmer. Kulia wanaofuatilia ni Kamishna wa
Madini Mhandisi David Mulabwa na Katibu wa Waziri, Kungulu Kasongi.
Kamishna wa Madini David Mulabwa
akizungumza jambo wakati wa kikao baina ya Waziri wa Madini Doto Biteko
na Rais wa Kampuni ya Amtec Resources Management Ltd ya nchini
Uingereza, Dkt. Peter Gollmer.
…………………………….
Waziri wa Madini Doto Biteko
amekutana na Rais wa Kampuni ya Amtec Resources Management Ltd ya nchini
Uingereza, Dkt. Peter Gollmer ambaye amemweleza Waziri Biteko kuhusu
ujio wa kampuni zipatazo 3 kutoka mataifa mbalimbali zenye nia ya
kuwekeza katika sekta ya madini.
Dkt. Gollmer amesema kampuni hizo
zimeonesha nia ya kuwekeza katika sekta ya madini hususan katika masuala
ya utafiti na uchimbaji wa madini kutokana na ushawishi unaofanywa na
Balozi wa Tanzania nchini Urusi Meja Jenerali Mstaafu Simon Mumwi
ambaye amekuwa akihamasisha watu wa mataifa mbalimbali nchini humo
kuwekeza nchini.
Pia, ameeleza kwamba, kampuni hizo
hazina shaka ya kuwekeza Tanzania kutokana na mazingira tulivu ya
kisisasa yaliyopo nchini pamoja na utajiri wa rasilimali madini ambayo
Tanzania imejaliwa kuwa nayo.
Akizungumza katika kikao hicho,
Waziri Biteko amemweleza Dkt. Gollmer kuwa kikao hicho ni muhimu na
kwamba milango kwa ajili ya wawekezaji wenye dhamira ya dhati ya
kuwekeza nchini iko wazi na kuongeza kuwa, kama wizara inaratajia
kukutana na kampuni hizo.
Wengine walioshiriki kikao hicho
ni Kamishna wa Madini Mhandisi David Mulabwa, Mkurugeni wa Idara ya Sera
na Mipango, Augustine Ollal na Katibu wa Waziri Kungulu Kasongi.
Post A Comment: