Na WAMJW-DOM.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amesema kuwa Serikali imefanukiwa kuokoa
kiasi cha Shilingi Bilion 3.4 ambacho kingetumika katika matibabu kwa
Wagonjwa wa Figo nje ya Nchi.
Dkt. Ndugulile ameyasema hayo leo Machi 14 wakati akiongea
na Waandishi wa Habari katika Ofisi za Wizara ya Afya Jijini Dodoma
ikiwa ni Siku ya Figo Duniani ambayo inaongozwa na kauli mbiu ya Afya ya
figo kwa kila mmoja kila.
Dkt. Ndugulile amesema kuwa Serikali imeokoa kiasi cha
shilingi bilioni 4.2 ambacho kingetumika katika matibabu ya wagonjwa 80
mpaka 100 ambao wangepelekwa nje ya nchi kwaajili ya matibabu.
“Wagonjwa waliokwishapandikizwa figo hapa nchini ni 42,
kama tungewapeleka wagonjwa nje ya nchi ingegharimu serikali kiasi cha
shilingi bilioni 4.2 kwa idadi hiyo ya wagonjwa. 80 mpaka 100, wakati
huduma hii hapa nchini inagharimu kiasi cha shilingingi milioni 21 kwa
kila mgonjwa.” Alisema Dkt. Ndugulile
Aidha, Dkt, Ndugulile amesema kuwa miongoni mwa sababu
zinazochangia magonjwa ya figo ni pamoja na uzito wa kupindukia
(obesity), matumizi makubwa ya sigara, unywaji wa pombe, uvutaji wa
sigara,kutokufanya mazoezi na kunywa madawa kiholela hasa dawa za
kupunguza maumivu.
Aliendelea kusema kuwa, magonjwa ya kisukari na shinikizo
la damu ni magonjwa yanayoongoza kwa kusababisha matatizo ya figo,
magonjwa haya yakitambuliwa mapema yanaweza kudhibitiwa kwa matibabu na
kuepusha madhara kwenye figo.
Kwa upande mwingine Dkt. Ndugulile amesema kuwa Kufikia
Desemba mwaka 2018, jumla ya vituo 28 vyenye jumla ya wagonjwa 1050
vilikuwa vikitoa huduma ya usafishaji damu katika mikoa ya Dar es
Salaam, Mwanza, Mbeya, Arusha, Kilimanjaro na Dodoma.
Mbali na hayo, Dkt. Ndugulile amesema Serikali imepiga
hatua kubwa ya kuanzisha huduma za kupandikiza figo hapa nchini katika
hospitali ya Taifa Muhimbili na Hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari wa Figo
nchini Dkt. Onesmo Kisanga amesema kuwa Ugonjwa wa Figo ni tatizo kubwa
nchini huku wananchi wengi wakiwa na uelewa mdogo juu ya athari na
visababishi vya ugonjwa huo.
Aidha Dkt. Onesmo amewataka wananchi kuacha tabia ya kunywa
dawa bila kupata ushauri wa kitaalamu hivyo kuepuka kuzalisha sumu
mwilini na kupelekea ugonjwa wa figo.
Hata hivyo Dkt. Onesmo Kisanga ameishukuru Serikali kwa kuwaendeleza kimasomo wataalam kwenye upande wa matibabu ya figo ambao sasa wamesambazwa sehemu mbali mbali ndani ya nchi kutoa huduma za matibabu.
Hata hivyo Dkt. Onesmo Kisanga ameishukuru Serikali kwa kuwaendeleza kimasomo wataalam kwenye upande wa matibabu ya figo ambao sasa wamesambazwa sehemu mbali mbali ndani ya nchi kutoa huduma za matibabu.
Naye Dkt. Grace Maghembe Kaimu Mkurugenzi wa Tiba kutoka
Wizara ya Afya amesema ungojwa huu umekuwa ukiwaathiri zaidi wakazi wa
mijini kuliko vijijini kutoka na mfumo wa maisha uliopo sasa ambapo watu
wengi wamekuwa hawazingatii mtindo bora wa maisha kwa kutofanya mazoezi
pamoja na kula chakula bora.
Dkt. Maghembe amesema bado ipo changamoto kwenye matumizi
ya dawa za mitishamba ambazo bado hazijatambuliwa na kuthibitishwa huku
akiwataka wananchi kuwa waangalifu pia kwenye matumizi ya dawa hizo.
“Serikali inatambua umuhimu wa tiba mbadala pamoja na
matibabu ya tiba za asili na ndio maana zipo taasisi za serikali
zinazohusika kuzitambua dawa hizo ni zipi na zina vitu gani na unatakiwa
kutumia kwa kiwango gani” amesema Dkt Maghembe nakuwataka watengenezaji
wa dawa hizo kufuata taratibu zilizopo ili kuthibitisha na kusajili
dawa zao.
Post A Comment: