Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel amewataka wananchi hususan wafugaji kutotumia matamko ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli vibaya kwa kutafuta mianya ya kutolipa kodi.

Akizungumza na wananchi mara baada ya kufanya ziara hiyo Prof. Gabriel amesema Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika kipindi cha mwezi mmoja itashirikiana na uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli kutoa tafsiri sahihi ya mfanyabiashara mdogo anayestahili kukatiwa kitambulisho cha biashara ndogo ndogo (machinga) cha Tsh. 20,000 kwa mwaka, kilichotolewa na Rais Magufuli kutokana baadhi ya wafugaji kutaka kufahamu endapo wanastahili kupatiwa vitambulisho.

“Mheshimiwa Rais alikuwa amelenga hasa wale wafanyabiashara wadogo wadogo na tunachoamini tutaendelea kulifanyia kazi lakini suala la machinga kwamba naye mfanyabiashara wa ng’ombe kuhusishwa katika sifa za mfanyabiashara ndogondogo bado ni gumu kulitolea majibu, lakini ushauri tusitumie matamko ya rais vibaya tusitafute kichaka cha kujificha kwamba nawe ni machinga, wewe mwenyewe fikiria na jitafakari tulipe kodi na tujenge nchi yetu.” Alisema Prof. Gabriel

Akizungumza na wafugaji hao Prof. Gabriel amepokea kilio cha wafugaji kuwa wamekuwa wakiuza ng’ombe kwa makadirio au matakwa ya mnunuzi kutokana na kutokuwepo kwa mizani ili waweze kuuza ng’ombe kwa kilo badala ya bei ya kukadiria kati ya mfugaji na mnunuzi wa ng’ombe, kitendo ambacho wafugaji hao wamesema kimekuwa kikiwafanya wasiuze mifugo yao kwa bei yenye tija kwao
Share To:

msumbanews

Post A Comment: